Algeria kumshitaki kocha wa Taifa Stars Charles Boniface Mkwasa, sababu ndio hii ..
November 17 timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars ilicheza mchezo wake wa pili wa kuwania kufuzu michuano ya Kombe la Dunia mwaka 2018 Urusi dhidi ya timu ya taifa ya Algeria mjini Blida katika uwanja wa Mustapha Tchaker, ikiwa ni siku tatu tu zimepita toka wacheze mchezo wa kwanza wa kuwania kufuzu michuano hiyo uwanja wa Taifa Dar Es Salaam na kumalizika kwa sare ya goli 2-2.
Mchezo wa pili uliyochezwa mjini Blida ulimalizika kwa Algeria kuibuka na ushindi wa goli 7-0 ila kabla ya mchezo huo kuanza waalgeria wana mtuhumu Mkwasa kutoa kauli za kibaguzi, hivyo wamepanga kumshitaki kwa shirikisho la mpira wa miguu ulimwenguni FIFA kwa kusema wao ni wabaguzi wa rangi.
Kupitia kwa mwenyekiti wa chama cha wanasoka Algeria Ahmed Boudry ameamua kumshitaki Mkwasa kwa kuwakosea heshima Algeria. Ahmed Boundry
>>> ” “Alisema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari
hata kabla ya mechi ambayo Tanzania ilifungwa goli saba. Tunaamua
kumfikisha FIFA kwa kuwa amewadhalilisha raia wote wa Algeria wakiwemo wachezaji”
CHANZO CHA STORI HII:SALEHJEMBE
Category: tanzania
0 comments