Ratiba ya Sportpesa super Cup hii hapa ....
Michuano ya Sportpesa Super Cup inayoshirikisha timu nane inategemewa kuanza kesho Uwanja wa Uhuru ambapo timu ya Singida United itashuka dimbani kuvaana na AFC Leopards kutoka Kenya katika robo fainali itakayochezwa kuanzia saa nane mchana.
Michuano ya robo fainali kesho itachezwa kwa awamu mbili na mechi ya pili itapigwa kuanzia saa kumi na robo jioni ambapo Mabingwa wa Ligi Kuu Bara Yanga watashuka dimbani kukipiga na Tusker FC kutoka nchini Kenya.
Baada ya michezo ya kesho Jumatatu siku ya Jumanne ya tarehe 6/06/2017 michuano ya robo fainali itaendelea kwa kuwakutanisha Mabingwa wa Kombe la Shirikisho nchini Simba Sports Club na timu ya Nakuru AllStars kutoka nchini Kenya, mchezo ambao utapigwa uwanja wa Taifa kuanzia saa nane mchana na mechi ya pili itakuwa saa kumi na robo ambapo itawakutanisha Gor Mahia ya Kenya na Jang'ombe Boys FC kutoka Zanzibar
Nusu Fainali ya michuano ya Sportpesa Super CUP itakuwa tarehe 8/06/2017
Category: tanzania
0 comments