HII NDIYO SIKU YA KUWASILI HAPA NCHINI KWA KOCHA MPYA WA TAIFA STARS NA SIKU ATAKAYOANZA KAZI RASMI

Nooij (59) atawasili saa 7.20 usiku kwa ndege ya Ethiopia Airlines ambapo anatarajia kukutana na waandishi wa habari Jumamosi mchana, saa chache kabla ya kuanza mechi ya kirafiki kati ya Taifa Stars na Burundi itakayochezwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Mart Nooij ni raia wa Uholanzi, na ameshawahi kufanya kazi katika nchi ya Mozambique kama kocha mkuu wa timu ya taifa, Burkina Faso U20, na pia ameifundisha timu ya Santos ya Afrika ya Kusini.
Category: tanzania
0 comments