Kocha wa Chelsea Jose Mourinho atoa msimamo mkali

Unknown | 9:55 PM | 0 comments

 


Kocha wa klabu ya Chelsea ya Uingereza Jose Mourinho bado yupo katika wakati mgumu wa kuhakikisha timu yake inafanya vizuri licha ya kuwa matumaini ya kutetea taji lake la Ligi Kuu Uingereza msimu huu yamepotea kwa kiasi kikubwa, Mourinho kwa sasa anatajwa kuwa hatarini kupoteza kibarua chake kutokana na mwenendo mbovu wa kikosi chake.
November 20 Jose Mourinho amefunguka na kueleza msimamo wake kuhusu dirisha dogo la usajili la mwezi January, wengi huenda wakafikiri kuwa kocha huyo atasajili mwezi January ili kuboresha kikosi chake lakini ana msimamo tofauti kidogo na wengi wanavyofikiria, Mourinho hana mpango wa kumuomba mmiliki wa Chelsea Roman Abramovich kutenga fungu la usajili.
Walsall-vs-Chelsea
“Sitaomba uongozi ufanye chochote katika dirisha la usajili la mwezi January nakiamini kikosi changu, sihitaji klabu itumie fedha kwa ajili ya usajili mwezi January, nafikiri tutacheza vizuri na kupata matokeo, tunaamini mambo mazuri yapo kwa ajili yetu” >>> Jose Mourinho
Klabu ya Chelsea katika dirisha la usajili la mwezi August iliwasajili  Pedro, Abdul Baba Rahman na Asmir Begovic pamoja na kumchukua kwa mkopo Radamel Falcao lakini hadi sasa imecheza mechi 12 na kupoteza mechi 7, imeshinda 3 na kutoa sare 2 na ipo nafasi ya 16 katika msimamo wa Ligi Kuu Uingereza kwa sasa kabla ya Jumamosi ya November 21 kucheza mechi yake ya 13 dhidi ya Norwich City.

Share story hii kupitia>>>>>> :
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

Category:

0 comments