SAKATA LA JUMA NYOSSO LACHUKUA SURA MPYA
Stori za beki wa kati na nahodha wa klabu ya Mbeya City aliyewahi kutamba na Simba Juma Nyosso amerudi katika headlines November 27, baada ya Chama cha Wachezaji Soka Tanzania (Sputanza) kuwasilisha ombi la kuomba Shirikisho la soka Tanzania (TFF) kupitia upya hukumu ya Juma Nyosso.
Katibu mkuu wa Sputanza Abeid Kasabalala amethibitisha kuwasilishwa kwa ombi hilo TFF na kupitia kwa afisa mtendaji mkuu wa bodi ya Ligi Boniface Wambura wamethibitisha kuridhia kupitia upya hukumu ya Juma Nyosso, bali hiyo sio rufaa ni ombi ambalo Sputanza wamewasilisha sambamba na kulipa Tsh 500,000/= ili ipitiwe upya adhabu ya Nyosso kwani ni kubwa sana kwa mchezaji.
Juma Nyosso alifungiwa
kucheza soka miaka miwili na kutakiwa kulipa faini ya Tsh milioni 2
baada ya kumfanyia kitendo cha kidhalilishaji nahodha wa Azam FC John Bocco September 27 katika mchezo kati ya Mbeya City dhidi ya Azam FC uliyochezwa katika dimba la Azam Complex Chamazi na Azam FC kuibuka na ushindi wa goli 2-1.
CHANZO CHA HII STORI:SALEHJEMBE
Category: tanzania
0 comments