MAN UNITED YAJIWEKA PAGUMU ULAYA, REAL MADRID YAJIFARIJI KWA USHINDI WA UGENINI

Unknown | 4:04 PM | 0 comments



MATOKEO NA RATIBA LIGI YA MABINGWA ULAYA
Novemba 25, 2015
Manchester United 0-0 PSV 
Malmo FF 0-5 Paris Saint-Germain
Atletico Madrid 2-0 Galatasaray
Shakhtar Donetsk 3-4 Real Madrid
Borussia Monchengladbach 4-2 Sevilla
Juventus 1-0 Manchester City
CSKA Moscow 0-2 VfL Wolfsburg
FC Astana 2-2 Benfica
Novemba 24, 2015
Bayern Munich 4-0 Olympiakos
Arsenal 3-0 Dinamo Zagreb
Barcelona 6-1 Roma
Lyon 1-2 KAA Gent
FC Porto 0-2 Dynamo Kyiv
Maccabi Tel Aviv 0-4 Chelsea
Zenit St Petersburg 2-0 Valencia CF
BATE Borisov 1-1 Bayer 04 Leverkusen
Wachezaji wa Manchester United, Jesse Lingard (kushoto) na Wayne Rooney (kulia) wakionyesha masikitiko yao baada ya sare na PSV PICHA ZAIDI GONGA HAPA

MANCHESTER United imelazimishwa sare ya 0-0 na PSV katika mchezo wa Kundi B Ligi ya Mabingwa Ulaya Uwanja wa Old Trafford.
Matokeo hayo, sasa yanaiweka katika nafasi ngumu United kwenda 16 Bora baada ya kufikisha pointi nane katika nafasi ya pili, ikizidiwa moja na vinara, VfL Wolfsburg na ikiwazidi moja PSV.
United sasa italazimika kushinda mechi yake ya mwisho dhidi ya Wolfsburg ili kusonga mbele.
Mechi nyingine ya kundi hilo, VfL Wolfsburg wameshinda 2-0 ugenini dhidi ya CSKA Moscow mabao ya Andre Schurrle dakika ya 67 na 88.

Mario Mandzukic ameifungia bao pekee Juve dhidi ya Manchester City  PICHA ZAIDI GONGA HAPA

Juventus imeichapa 1-0 Manchester City nchini Italia katika mchezo wa Kundi D, bao pekee la Mario Mandzukic dakika ya 18. City na Juve zote zimejihakikishia kwenda 16 Bora.
Mchezo mwingine wa kundi hilo, Borussia Monchengladbach imeshinda 4-2 dhidi ya Sevilla. Mabao ya Monchengladbach yamefungwa na Lars Stindl mawili, Fabian Johnson na Raffael Caetano de Araujo, wakati ya Sevilla yamefungwa na Victor Machin Perez na Ever Banega kwa penalti.
Real Madrid imepata ushindi wa 4-3 ugenini dhidi ya Shakhtar Donetsk mchezo wa Kundi A mabao yake yakifungwa na Cristiano Ronaldo mawili dakika ya 18 na 70, Luka Modric dakika ya 50 na Daniel Carvajal dakika ya 52, wakati ya wenyeji yamefungwa na Alex Teixeira kwa penalti dakika ya 77 na 88 na Bruno Ferreira Bonfim dakika ya 83.
Ronaldo akikimbia kushangilia baada ya kuifungia Real Madrid  PICHA ZAIDI GONGA HAPA

Mchezo mwingine wa kundi hilo, PSG imeshinda 5-0 ugenini dhidi ya Malmo FF, mabao ya Adrien Rabiot, Angel Di Maria mawili, Zlatan Ibrahimovic na Lucas Rodrigues Moura da Silva.
Atletico Madrid imeshinda 2-0 dhidi ya Galatasaray mchezo wa Kundi C, mabao ya 
Antoine Griezmann dakika ya 13 na Antoine Griezmann dakika ya 65, wakati mchezo mwingine wa kundi hilo, FC Astana na Benfica zimetoka sare ya 2-2.
 
Binzubery online

Share story hii kupitia>>>>>> :
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

Category:

0 comments