Mchezaji wa Kibrazil Andry Coutinho amevunja mkataba wake na Yanga, sababu amekiuka haya …

Unknown | 10:01 PM | 0 comments

 


Headlines ya zile tetesi za klabu ya Dar Es Salaam Young African kumtema kiungo wa kimataifa wa Brazil aliyekuwa anakipiga katika klabu hiyo Andry Coutinho zimekuwa tofauti na vile ambavyo wengi walikuwa wakifikiria, uongozi wa klabu ya Yanga kupitia kwa afisa habari wake Jerry Muro wamethibitisha hilo.
Kiungo huyo wa kimataifa wa Brazil anatajwa kuvunja mkataba wake baada ya kuondoka na kwenda kwao Brazil kwa mapumziko baada ya kusimama kwa Ligi hadi December 12 ili kupisha mechi za michuano ya kimataifa pamoja na Kombe la CECAFA Challenge lakini hajarea Tanzania kwa ajili ya kuendelea na mazoezi bila kuwa na ruhusa ya klabu hivyo Yanga itamchukulia hatua stahiki.
HMB_6496
“Coutinho ameondoka lakini taratibu za kuondoka kwake hakufuata kanuni za mkataba wake na Yanga, kwani aliondoka hadi hivi sasa hajarudi na sisi tunatafakari kwa kina sana, ila liwalo na liwe kama hayupo tunatafuta mbadala wake, hatuwezi kukaa na kusubiria mchezaji ambaye hatujui anarudi lini lakini kikanuni amevunja mkataba wake na klabu” >>> Jerry Muro

Share story hii kupitia>>>>>> :
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

Category:

0 comments