Haya ndio majina ya wachezaji 40 waliochaguliwa kuwania nafasi kuunda kikosi bora cha UEFA 2015 …
November 24 shirikisho la soka barani Ulaya UEFA limetangaza majina 40 ya wachezaji wanaowania nafasi ya kuunda kikosi bora cha UEFA kwa mwaka 2015, UEFA
ambao wametangaza majina hayo 40 ambayo yatachujwa hadi kufikia 11
wametoa nafasi ya mashabiki duniani kote kupiga kura kuchagua kikosi
hicho kupitia tovuti yao.
Majina hayo 40 yametangazwa wakati vilabu vya Man United na Liverpool havijatoa mchezaji hata mmoja katika list hiyo lakini Ligi Kuu Uingereza imetoa wachezaji watano tu katika list hiyo ambao ni Eden Hazard, Kevin De Bruyne, Alexis Sanchez na Sergio Aguero na golikipa Joe Hart wakati FC Barcelona wametoa wachezaji nane katika list hiyo.
Magolikipa
Joe Hart (Manchester City), Gianluigi Buffon (Juventus), Manuel Neuer (Bayern Munich), Denys Boyko (Dnipro)
Mabeki
Leonardo Bonucci (Juventus), David Alaba (Bayern Munich), Giorgio Chiellini (Juventus), David Luiz (Paris Saint-Germain), Dani Alves (Barcelona), Thiago Silva (Paris Saint-Germain), Jerome Boateng (Bayern Munich), Ricardo Rodriguez (Wolfsburg), Javier Mascherano (Barcelona), Diego Godin (Atletico Madrid), Gerard Pique (Barcelona), Sergio Ramos (Real Madrid)
Viungo
Grzegorz Krychowiak (Sevilla), Kevin De Bruyne (Manchester City), Ivan Rakitic (Barcelona), Arturo Vidal (Bayern Munich), Eden Hazard (Chelsea), Claudio Marchisio (Juventus), Marco Verratti (Paris Saint-Germain), Yevhen Konoplyanka (Sevilla), Andres Iniesta (Barcelona), James Rodriguez (Real Madrid), Paul Pogba (Juventus), Hakan Calhanoglu (Bayer Leverkusen).
Washambuliaji
Gareth Bale (Real Madrid), Thomas Muller (Bayern Munich), Lionel Messi (Barcelona), Zlatan Ibrahimovic (Paris Saint-Germain), Robert Lewandowski (Bayern Munich), Neymar (Barcelona), Antoine Griezman (Atletico Madrid), Alvaro Morata (Juventus), Sergio Aguero (Manchester City), Luis Suarez (Barcelona), Alexis Sanchez (Arsenal), Cristiano Ronaldo (Real Madrid).
Category: uingereza
0 comments