Haya ndio majina matano ya makocha wanaotajwa kumrithi Rafael Benitez licha ya Real Madrid kuficha …
Headlines za kipigo cha goli 4-0 ilichokipata Real Madrid katika uwanja wake wa nyumbani dhidi ya wapinzani wao wa jadi FC Barcelona bado kipo katika headlines za soka hadi leo hii November 24. Jioni ya November 23 uongozi wa klabu ya Real Madrid ukiongozwa na Rais wa klabu hiyo Fiorentino Perez ulifanya kikao na kuja na majibu ya kuendelea kumuunga mkono kocha wa timu hiyo Rafael Benitez.
Hata hivyo uamuzi wa Real Madrid kutangaza jioni ya November 23 kuwa wanamuunga mkono kwa asilimia 100 kocha wao Rafael Benitez ambaye alikuwa anatajwa kuwa kama akifungwa mechi dhidi ya FC Barcelona atafukuzwa kazi, bado zinatajwa kuwa ni danganya toto. Stori zilizoandikwa November 24 katika mtandao wa mirror.co.uk kuwa bado Benitez anatajwa kufukuzwa kwa siku za usoni.
Benitez atafukuzwa na tayari majina matano kwa habari za kichunguzi zinatajwa kuwa makocha watano wanatajwa kurithi nafasi ya Benitez ambaye anaaminika kuwa mbinu zake sio nzuri. Majina matano yanayotajwa kurithi nafasi ya Benitez ni kocha wa sasa wa Chelsea Jose Mourinho, Zinedine Zidane, Leonardo Jardim, Joachim Löw na Carlo Ancelotti ambaye aliwahi kuifundisha klabu hiyo.
Category: uingereza