Kavumbagu kumpisha Traore Azam FC
Ibrahim Mussa,
Dar es Salaam
IMEVUJA! Licha ya kuwepo kwa taarifa za straika wa Azam FC, Mrundi, Didier Kavumbagu kutakiwa nchini Sweden lakini inadaiwa kuwa uongozi wa timu hiyo umepanga kumtoa kwa mkopo ili kumpisha mshambuliaji Mohammed Traore raia wa Mali anayeichezea El Merreikh ya Sudan.
Licha ya Kavumbagu kufunga mabao matatu katika mechi mbili alizoichezea Azam msimu huu, anaonekana hana furaha ndani ya timu hiyo kutokana na kutokuwa na uhakika wa nafasi katika kikosi cha kwanza.
Awali, msimu uliopita katika kipindi cha dirisha dogo, uongozi wa timu hiyo ulikuwa kwenye mpango wa kumsajili Traore kabla ya mipango hiyo kutibuka kutokana na kung’ang’aniwa na timu yake ya El Merreikh, kwani ndiye tegemeo lao ambaye alikuwemo kwenye kikosi cha Mali kilichocheza Fainali za Mataifa ya Afrika (Afcon) mwaka jana nchini Guinea ya Ikweta.
Mtu wa karibu na Kavumbagu alisema kwa sasa uongozi wa Azam upo katika mikakati kabambe ya kuhakikisha inamtoa kwa mkopo Kavumbagu ili kuweza kufanikisha mpango wao wa kumsajili Traore kabla ya dilisha dogo la usajili kufungwa Desemba 15, mwaka huu.
Championi lilimtafuta Katibu Mkuu wa Azam FC, Idrissa Nassor ambaye alifunguka: “Kavumbagu bado tuna mkataba naye ambao umebaki miezi sita lakini tupo tayari kumuuza kwenda timu yoyote itakayokuwa inamhitaji na siyo vinginevyo, kwa sababu ni mchezaji wetu halali kisheria.”

Category: tanzania
0 comments