Aibu…Nd’aw aondoka Bongo na Sh milioni 3

Unknown | 6:55 PM | 0 comments

 

ABDOULAYE-NDAW
straika Msenegali, Pape N’daw.
Nicodemus Jonas
na Wilbert Moland
USIBISHE ukweli ndiyo huo! Rasmi mwishoni mwa wikiendi hii, Simba ilimalizana na straika Msenegali, Pape N’daw kwa kusitisha mkataba wake, lakini tofauti na ilivyozoeleka mastaa kuchota mamilioni ya fedha, kwa N’daw ni tofauti.

Straika huyo alisitisha mkataba wa mwaka mmoja aliousaini mwanzoni mwa msimu huu, hata hivyo Simba iliamua kuachana naye kutokana na kutokuwa na msaada wowote zaidi ya kuitia doa kwa matukio ya aibu.
Habari za ndani, zinasema nyota huyo ameambulia kupewa dola 3, 000 ambazo ni sawa na Sh 6,356,730, kwa kuvunja mkataba, lakini makubaliano yao ni kwamba angejigharamikia kila kitu kuhusu safari ya kurudi kwao.
Kwa mujibu wa Tovuti ya Farecompare, nauli ya kutoka Dar es Salaam kwenda Dakar, Senegal ni dola 1,347, sawa na Sh 2,854,170 kwa Shirika la Ndege la Kenya Airways, kwamba iwapo N’daw atatumia kampuni hiyo, atabakisha kiasi cha dola 1,653 ambazo ni sawa na Sh 3,502,560.
Mratibu wa Simba, Abbas Ally ‘Gazza’, ameliambia Championi Jumatatu: “Tulishamalizana naye na alikuwa aondoke kati ya Jumamosi usiku au Jumapili (jana). Kuhusu makubaliano hiyo ni siri ya klabu na mchezaji mwenyewe, cha msingi kwa cheo changu naweza kukwambia N’daw hatutakuwa naye tena kwenye kikosi basi.”
Wakati Msenegal huyo akirejea Senegal na hela hiyo ndogo, imebainika kuwa Simon Sserunkuma, raia wa Uganda, yeye alikunja kitita cha dola 5,000, sawa na Sh 10,594,600 kwa kukatisha mkataba wiki iliyopita.
Katika mkwanja wake huo, alimega kiasi cha dola 200, sawa na Sh 423,782 kuchukua ndege ya kumrusha Kampala mara moja na kuanza maisha mapya.


GPL

Share story hii kupitia>>>>>> :
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

Category:

0 comments