BARCA YAICHARANGA REAL MADRID
Ligi Kuu Hispania imeendelea tena leo November 21 kwa kuzikutanisha timu kadhaa kucheza mechi zao za muendelezo wa Ligi Kuu Hispania, miongoni mwa mechi zilizochezwa November 21 ni mchezo wa watani wa jadi kati ya Real Madrid dhidi ya mahasimu wao FC Barcelona katika dimba la Santiago Bernabeu jijini Madrid.
Real Madrid na FC Barcelona kabla ya mchezo huu wa kihistoria kuchezwa walikuwa wamepishana kwa tofauti ya point tatu, Real Madrid
wakiwa nyuma kwa kupoteza mchezo mmoja, huu ndio mchezo ambao kwa sasa
una rekodi za kuangaliwa na watu wengi duniani. Licha ya kuwa Real Madrid wanaongoza kwa takwimu ya kumfunga FC Barcelona mara 92 kwa 89 hawakuweza kutamba katika uwanja wao wa nyumbani.
Mchezo ulianza kwa FC Barcelona kupiga pasi nyingi kama kawaida yao na dakika ya 8 Luis Suarez akaanza kuwapa furaha mashabiki wa FC Barcelona duniani kote kwa kufunga goli la kwanza, wakati ambao Real Madrid wanajipanga namna ya kusawazisha goli hilo Neymar akapachika goli la pili dakika ya 39 na kwenda mapumziko wakiwa mbele kwa goli 2-0.
Kipindi cha pili kilianza kwa FC Barcelona kuendelea kumiliki mpira hadi dakika ya 52 Andre Iniesta, FC Barcelona ambao dakika 4 baada ya Iniesta kufunga goli la tatu walimuingiza Lionel Messi kuchukua nafasi ya Ivan Rakitic ambaye alienda kuongeza nguvu na dakika ya 73 Luis Suarez akapachika goli la nne. Hadi dakika 90 zinamalizika FC Barcelona 4-0 Real Madrid.
Category: uingereza
0 comments