WANAOWANIA TUZO BORA ZA SOKA ZA DUNIA HAWA HAPA ......
WINGA
wa Wales, Gareth Bale ni Muingereza pekee aliyepenya katika orodha ya
wachezaji 23 wanaowania tuzo ya Mwanasoka Bora wa Dunia, Ballon d'Or kwa
mwaka wa tatu mfululizo.
Bale
ni miongoni mwa wachezaji 11 wanaocheza Ligi Kuu ya Hispania, maarufu
kama La Liga walioingia katika orodha hiyo ambayo ina wengine watano wa
Ligi Kuu ya England na watano wa Ligi Kuu ya Ujerumani, Bundesliga.
Wachezaji
watatu wa Manchester City, Sergio Aguero, Kevin De Bruyne na Yaya Toure
wameingia kwenye orodha hiyo sambamba na winga wa Chelsea, Eden Hazard
na Alexis Sanchez, ambaye amekuwa na mchango mkubwa katika klabu yake,
Arsenal na kuipa mafanikio timu yake ya taifa, Chile katika Copa America
mwaka 2015.
Mshambuliaji wa Real Madrid, Gareth Bale ni Muingereza pekee aliyeingia katika orodha ya Mwanasoka Bora wa Dunia, Ballon d'Or PICHA ZAIDI GONGA HAPA
Mfaransa
Arsene Wenger na Mreno Jose Mourinho wote wameingia kwenye 10 bora ya
tuzo za kocha bora wa dunia, sambamba na kocha wa mabingwa wa Ulaya,
Barcelona Luis Enrique na wa Bayern Munich, Pep Guardiola.
Kocha
wa Chile, Jorge Sampaoli ni kocha pekee wa timu ya taifa kwenye orodha
hiyo, ambayo pia inahusisha makocha wa Juventus, Massimiliano Allegri,
Unai Emery wa Sevilla, Laurent Blanc wa PSG, Diego Simeone wa Atletico
Madrid na Carlo Ancelotti, aliyeondoka Real Madrid baada ya msimu
uliopita.
Kocha wa Chelsea, Jose Mourinho ameingia kwenye orodha ya kuwania tuzo ya kocha bora wa mwaka
Category: uingereza
0 comments