MAN UNITED, MAN CITY ZANG’ARA ULAYA, RONALDO AVUNJA REKODI YA RAUL, REAL IKIUA 2-0

Unknown | 8:57 AM | 0 comments



Wachezaji wa Manchester United wakishangilia na Smalling aliyefunga bao la ushindi dhidi ya Wolfsburg PICHA ZAIDI GONGA HAPA

MANCHESTER United imepata ushindi mwembamba wa mabao 2-1 dhidi ya VfL Wolfsburg ya Ujerumani katika mchezo wa Kundi B Ligi ya Mabingwa Ulaya, Uwanja wa Old Trafford usiku huu.
United walilazimika kutoka kupata ushindi huo, kwa mabao ya Juan Mata kwa penalti dakika ya 34 na Chris Smalling dakika ya 53, baada ya Daniel Caligiuri kutangulia kuifungia Wolfsburg dakika ya nne.
Mchezo mwingine wa Kundi B, CSKA Moscow imeshinda 3-2 dhidi ya PSV, mabao yake yakifungwa na Ahmed Musa dakika ya nane na Seydou Doumbia mawili dakika ya 21 na 36 kwa penalti, wakati ya PSV yamefungwa na Maxime Lestienne dakika ya 60 na 68 Uwanja wa Arena Khimki.
Sergio Aguero (centre) wheels away in celebration after scoring a last-minute penalty to secure the win for Manchester City in Germany
Sergio Aguero (katikati) akikimbia kushangilia baada ya kuifungia kwa penalti Manchester City Ujerumani PICHA ZAIDI GONGA HAPA
Mwanasoka bora wa dunia, Cristiano Ronaldo amefanikiwa kufikia rekodi ya mabao ya Raul katika Ligi ya Mabingwa Ulaya, baada ya kuifungia mabao yote, Real Madrid ikishinda 2-0 ugenini dhidi ya Malmo FF dakika ya 29 na 90 Uwanja wa Swedbank mchezo wa Kundi A.
Ronaldo amefikisha mabao 82 katika Ligi ya Mabingwa na mabao 501 jumla tangu aanze kucheza soka pamoja na kumfikia kwa mabao gwiji wa Real, Raul aliyekuwa anaongoza kuifungia mabao mengi klabu hiyo.
Mchezo mwingine wa Kundi A, Shakhtar Donetsk imefungwa mabao 3-0 na Paris Saint-Germain nyumbani mabao ya Serge Aurier, David Luiz Moreira Marinho na Darijo Srna la kujifunga Uwanja wa Arena Lviv.
Juventus imeshinda 2-0 dhidi ya Sevilla mchezo wa Kundi D Uwanja wa Juve, mabao ya Alvaro Morata dakika ya 41 na Simone Zaza dakika ya 87.
Mchezo mwingine wa kundi hilo, Manchester City wameshinda ugenini mabao 2-1 dhidi ya Borussia Monchengladbach Uwanja wa Borussia-Park. Mabao ya City yamefungwa na Nicolas Otamendi dakika ya 65 na Sergio Aguero kwa penalti dakika ya 90, huku bao la wenyeji likifungwa na Lars Stindl dakika ya 54.
Mchezo wa Kundi C, Atletico de Madrid imefungwa nyumbani 2-1 na Benfica licha ya kutangulia kwa bao la Angel Correa dakika ya 23, lakini waliibuka ‘kidedea’ kwa mabao ya Nicolas Gaitan dakika ya 36 na Goncalo Manuel Ganchinho Guedes dakika ya 51 Uwanja wa Vicente Calderon.
Real Madrid forward Cristiano Ronaldo celebrates his 81st Champions League goal against Malmo at the Swedbank Stadium
Mshambuliaji wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo akisherehekea bao lake Uwanja wa Swedbank PICHA ZAIDI GONGA HAPA
Mchezo mwingine wa kundi hilo, FC Astana imetoka sare ya 2-2 na Galatasaray. Mabao ya Astana yamefungwa na Hakan Balta aliyejifunga dakika ya 77 na Lionel Carole aliyejifunga pia dakika ya 89, wakati ya Galatasaray yamefungwa na Bilal Kisa dakika ya 31 na Nenad Eric aliyejifunga dakika ya 86.
 
credit: Bin Zubeiry

Share story hii kupitia>>>>>> :
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

Category:

0 comments