CHRISTIANO RONALDO 'CR7' AVUNJA REKODI YA KISOKA
Mshambuliaji
wa Real Madrid, Christiano Ronaldo akikabidhiwa kiatu cha dhahabu na
Rais wa timu hiyo, Florentino PĂ©rez wakati wa hafla ya kumpogeza
mchezaji huyo.
Christiano Ronaldo akiwa na mama yake na mwanaye.
Perez akiwahutubia wachezaji na viongozi wa Madrid
Ronaldo na Familia yake.(P.T)
Christiano Ronaldo akitoa neno.
Perez akiendelea kuzungumza
Tuzo mbalimbali alizojinyakulia Ronaldo
Ronaldo na wachezaji wenzake wa Madrid
...Ronaldo akionesha moja ya tuzo yake
Kikosi cha Madrid
Ronaldo akibusu kiatu cha dhahadu alichokabidhiwa kama tuzo.
SALEH ALLY
MSHAMBULIAJI
nyota duniani, Cristiano Ronaldo, amefikisha mabao 500 aliyoyafunga
akiwa na timu tatu pamoja na timu yake ya taifa.
Ronaldo
amefikisha mabao 500 katika kipindi ambacho ametimiza miaka 30, jambo
ambalo si dogo au si la kuliacha lipite tu. Hakika Ronaldo ambaye
amekuwa mwanasoka bora duniani mara tatu, ana kipaji cha juu kabisa.
Mabao hayo na mfano utaona amefikisha mabao 323 sawa na gwiji wa Real
Madrid, Raul Gonzalez si jambo dogo. Sasa ana nafasi ya kuwa gwiji kwa
kufunga mabao mengi zaidi.
Tayari
Ronaldo ana rekodi ya wastani wa juu zaidi katika ufungaji kwenye Ligi
Kuu Hispania ‘La Liga’. Ana wastani wa 1.05 ya mabao. Maana yake
amefunga bao katika kila mechi kama mabao yake yatagawanywa.
Mafanikio
ya mabao 500 tangu alipofunga bao lake la kwanza akiichezea Sporting
Lisbon ya Ureno Oktoba 7, 2002. Ndani ya miaka 13, Ronaldo ameweza
kufunga mabao hayo 500 tena akicheza katika timu kubwa tatu ambazo
hakika zinakuwa na ushindani wa juu na wachezaji wake hupambana na
upinzani wa juu kabisa. Ameshinda kila kombe kwa ngazi ya klabu akiwa na
Manchester United na Real Madrid ambazo ni moja ya timu kubwa tatu
zaidi duniani.
Wakati
anatua Real Madrid, msimu wa kwanza aliweza kuweka wastani wa mabao 20
kwa msimu. Baada ya hapo akapanda kwenda hadi mabao 53, kitu ambacho si
mzaha hata kidogo. Msimu wake wa kwanza naalifunga mabao 21, uliofuata
wa 2010/11 akatandika kimiani mabao 50. Msimu wa 2011/12, akafunga mabao
66, msimu wa 2012/13 akashuka kwa kufunga mabao 51, ule wa 2013/14
akafunga mabao 56 na 2014/15 akafunga mabao 66.
Angalia
ushindani wa La Liga au michuano ya Ulaya, lakini huyu mtu ana uwezo wa
kufunga hadi mabao 50 kwa zaidi ya misimu miwili au mitatu
anafanya
hivyo. Katika hali ya kawaida unaamini kweli ni kipaji pekee? Ndiyo
maana nikaamua kukumbusha kwamba mafanikio ya watu hawa hayapatikani
ukiwa umelala na kufumba macho.
Lazima
kujituma, lazima kujipambanua na kuamini mtafutaji hachoki. Historia ya
Ronaldo inajielezea, kwa kuwa wazazi wake walikuwa ni watu wa maisha ya
chini kabisa.
Baba yake
alikuwa ni mtunza bustani tu huko kwao katika Kisiwa cha Madeira,
Ureno. Ronaldo alionyesha anataka kufanikiwa na utaona wakati akiwa
Manchester United wachezaji wengi walimshangaa kwamba anaishi vipi,
kweli anaweza kula raha na maisha yake. Kwamba hakuwa akijipa nafasi ya
kula maisha? Maana alikuwa akifika mazoezini saa moja au mbili kabla ya
wenzake, aliondoka mazoezini saa moja baada ya wenzake. Muda wote
aliokuwa pale aliendelea kujifua zaidi. Hata walipokwenda gym, yeye
ndiye alibaki muda mwingi zaidi ya wengine. Kuna wakati hadi Kocha Sir
Alex Ferguson aliwahi kumuonya kufanya hivyo, kwamba apunguze mazoezi.
Wakati
anatokea Manchester United kwenda Madrid, wengi walichambua na kusema
angefunikwa kabisa na Lionel Messi na kupotea. Lakini leo amebaki pekee
anayechuana vikali na mshambuliaji huyo wa Barcelona mwenye kipaji cha
juu kabisa. Ronaldo si mashine, ni binadamu kama wewe lakini ameamua
kuishi tofauti, ameamua kutaka kufanikiwa. Amepania kutimiza ndoto zake
bila ya kusikiliza maneno mengi ya pembeni ambayo hukatisha tamaa.
Hii
inakuhusu wewe mchezaji wa soka wa Tanzania katika daraja lolote, achana
na woga na kusikilizasana maneno ya watu hasa yale yanayosisitiza
‘hauwezi’. Unaweza zaidi ya wanavyofikiri, unaweza kufika zaidi ya
ulipo. Lakini usifumbe macho ukalala. Hauwezi kuwa kama Ronaldo, lakini
unaweza kupata mafanikio ya juu yanayoweza kuwashangaza wengi kama Mreno
huyo anavyoshangaza kwa mabao yake hayo 500.
Kwa
Tanzania hata kufunga mabao 50 kwa misimu minne nayo ni shida kubwa.
Bado wewe unaweza kuwa wa kwanza kama utaachana na woga, kukubali
kukatishwa tamaa. Ronaldo si mashine, ni binadamu lakini anafanikiwa.
Lakini lazima ukubali kuumia zaidi na kujituma zaidi ili kufikia
mafanikio. Usiyaache mafanikio yake ya mabao 500 yapite tu kama kitu cha
kukushangaza, badala yake yafanyie kazi siku nyingine yakusaidie hata
katika maisha ya kawaida. Panga ndoto, iote ukipambana na mwisho
ufanikiwe.
BAO LA KWANZA AKIWA….
SPORTING LISBON
Oktoba 7, 2002 vs Real Betis.
MAN UNITED
Novemba Mosi, 2003 vs Portsmouth.
REAL MADRID
Agosti 29, 2009 vs Deportivo.
TIMU YA TAIFA URENO
Juni 12, 2004 vs Ugiriki.
MABAO:
NDANI YA BOKSI: 417
NJE YA BOKSI: 83
PENALTI: 81
ADHABU: 45
ALIFUNGAJE?
Mguu wa Kulia: 326
Mguu wa kushoto: 89
Kichwa: 83
TIMU ALIZOZIFUNGA LA LIGA:
Sevila-21, Getafe-18, Barcelona-15,
Atletico Madrid-15, Malaga-14
WALIOMPA ‘ASISTI’ NYINGI:
Karim Benzema 31, Mesut Ozil 28,
Angel di Maria 20, Gareth Bale 15,
Ryan Giggs 16, Gonzalo Higuain 15.
Category: uingereza
0 comments