Muone Ronaldo akiwa katika ndege binafsi akielekea kujiunga na timu yake ya taifa…
Ikiwa ni mapumziko mafupi ya Ligi Kuu mbalimbali duniani ili kupisha michezo kadha ya timu za taifa iliyo katika kalenda za FIFA, Real Madrid ya Hispania ilimaliza mechi yake ya weekend kabla ya kwenda mapumziko mafupi dhidi ya Atletico Madrid na mechi kumalizika kwa sare ya goli 1-1, mshambuliaji wao Cristiano Ronaldo amekodi ndege binafsi kwenda kujiunga na timu yake ya taifa.
Cristiano Ronaldo ambaye alikuwa anahitaji goli moja tu ili avunje rekodi ya ufungaji wa muda wote wa klabu ya Real Madrid iliyokuwa inashikiliwa na Raul, amesafiri na ndege binafsi kuelekea kujiunga na kambi ya timu ya taifa ya Ureno, ambayo itacheza mechi mbili za kuwania kufuzu michuano ya mataifa ya Ulaya.
Licha ya Cristiano Ronaldo kutofanikisha lengo lake la kuwa mfungaji bora wa muda wote wa klabu ya Real Madrid, tayari ndio mchezaji wa timu ya taifa ya Ureno ambaye ndio mfungaji bora wa muda wote wa nchi hiyo, Cristiano Ronaldo
ana jumla ya goli 55 alizofunga akiwa na timu yake y taifa. Lakini
anatajwa kufunga zaidi ya magoli 500 ikiwa ni jumla ya goli alizofunga
katika vilabu alivyochezea na timu ya taifa.
Category: uingereza