MAN CITY NA LIVERPOOL ZAMSOGELEA ‘MWALI’ WA CAPITAL ONE ENGLAND, ARSENAL NJE

Unknown | 7:35 AM | 0 comments


MATOKEO NA RATIBA KOMBE LA LIGI ENGLAND:
Oktoba 28, 2015  

Manchester United (1) 0 - 0 (3) Middlesbrough

Manchester City 5 - 1 Crystal Palace

Liverpool 1 - 0 Bournemouth

Southampton 2 - 1 Aston Villa

Oktoba 27, 2015  

Sheffield Wednesday 3 - 0 Arsenal

Stoke City (5) 1 - 1 (4) Chelsea

Everton (4) 1 - 1 (3) Norwich City

Hull City (5) 1 - 1 (4) Leicester City

Desemba 1, 2015

Middlesbrough v Everton Riverside 

Southampton v Liverpool

Manchester City v Hull City

Stoke City v Sheffield Wednesday 

Nahodha wa Manchester City, Yaya Toure akifunga bao la nne jana dhidi ya Crystal Palace PICHA ZAIDI GONGA HAPA

MANCHESTER City na Liverpool zimekwenda Robo Fainali ya Kombe la Ligi England, maarufu kama Capital One Cup kufuatia ushindi kwenye mechi zao za jana usiku, huku Manchester United ikiungana na Arsenal kuaga michuano hiyo.

Manchester United imetolewa kwa penalti 3-1 na Middlesbrough baada ya sare ya 0-0 Uwanja wa Old Trafford, wakati Manchester City imeshinda 5-1 dhidi ya Crystal Palace Uwanja wa Etihad.

Mabao ya City yamefungwa na Wilfried Bony dakika ya 22, Kevin De Bruyne dakika ya 44, Kelechi Iheanacho dakika ya 59, Yaya Toure kwa penalti dakika ya 76 na Manuel Garcia Alonso dakika ya 90 na ushei, wakati bao la kufutia machozi la Palace limefungwa na Damien Delaney dakika ya 89.

Bao pekee la Nathaniel Clyne dakika ya 17 limeipa 

Liverpool ushindi wa 1-0 dhidi ya Bournemouth Uwanja wa Anfield, wakati Southampton imeichapa 2-1 Aston Villa mabao ya Maya Yoshida dakika ya 51 na Graziano Pelle dakika ya 77, bao la wageni likifungwa na Scott Sinclair kwa penalti dakika ya 90 na ushei Uwanja wa St. Mary's.

Mapema juzi, Sheffield Wednesday iliikung’uta 3-0 Arsenal, mabao ya Ross Wallace dakika ya 27, Lucas Eduardo Santos Joao dakika ya 40 na Sam Hutchinson dakika ya 51 Uwanja wa 
Hillsborough.
Chelsea nayo ilitolewa kwa penalti 5-4 baada ya sare ya 1-1 na Stoke City Uwanja wa Britannia. Stoke walitangulia kwa bao la Jonathan Walters dakika ya 52, kabla ya Loic Remy kusawazisha dakika ya mwisho.

Everton iliitoa Norwich City kwa penalti 4-3 baada ya sare ya 1-1 Uwanja wa Goodison Park na Hull City iliitoa Leicester City kwa penalty 5-4 baada ya sare ya 1-1 Uwanja wa The KC. 
 
Bin Zubeiry

Share story hii kupitia>>>>>> :
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

Category:

0 comments