Top 10 ya thamani ya tweet za wanamichezo, Cristiano Ronaldo kaongoza…
Umeshawahi kujiuliza kwa nini mshambuliaji wa kimataifa wa Ureno na klabu ya Real Madrid ya Hispania Cristiano Ronaldo hutumia account yake ya twitter kuitangaza kampuni ya nguo ya kwao Ureno, Unajua ni kwa nini Wayne Rooney hutangaza viatu vya Nike katika account yake ya twitter?
Kwa mujibu wa mtandao wa dailymail.com utafiti unaonyesha likes wanazopata Ronaldo, Rooney na Neymar kwa tweet moja wanayo tweet katika account zao, hulipwa fedha nyingi na kampuni zinazo wadhamini. Hivyo nakusogezea top 10 ya thamani ya tweet moja kwa mastaa hao.
Ripoti kutoka katika gazeti la Kihispania AS na kampuni ya mawakala wa matangazo ya Opendorse imethibitisha kuwa Cristiano Ronaldo mwenye followers milioni 37.7 katika mtandao wa twitter.
Post moja ya tangazo la biashara akipost katika account yake ina
thamani ya pound 169280 ambayo ni zaidi ya milioni 500 za Kitanzania.
Ronaldo anashika nafasi ya 13 kwa watu wenye followers wengi katika account ya twitter ni namba mmoja kwa wanamichezo wote.
Hii ni List ya Top 10 yote.
Category: uingereza
0 comments