ARGENTINA YACHAPA MTU 7-0
.
MSHAMBULIAJI
Sergio Aguero amefunga mabao mawili na kuseti matatu Argentina
ikiifumua Bolivia 7-0 usiku wa kuamkia leo katika mchezo wa kirafiki
Uwanja wa BBVA Compass mjini Houston.
Mwanasoka
Bora wa Ulaya, Lionel Messi amefunga mabaio mawili licha ya kuingia
dakika 65 akitokea benchi, huku Ezequiel Lavezze akifunga mawili pia na
linguine Angel Correa. Lavezzi alifunga dakika ya sita na 41, Aguero
dakika ya 34 na 59, Messi dakika ya 67 na 75, wakati Correa alishindilia
msumari wa mwisho kwenye jeneza la Bolivia dakika ya 84.
Kikosi
cha Argentina kilikuwa; Romero, Casco/Roncaglia dk77, Funes Mori,
Rodriguez, Mas, Pereyra, Kranevitter, Lamela/Banega dk77, Lavezzi/Correa
dk81, Aguero/Tevez dk80 na Gaitan/Messi dk65.
Bolivia;
Daniel Vaca, Raldes, Zenteno, Hurtado, Smedberg-Dalence/Ramallo dk65,
Danny Bejarano/Cabrera dk46, Melean/Lizio dk46, Cardozo/Eguino dk46,
Arce/Chumacero dk46, Martins na Veizaga
Category: uingereza
0 comments