Kumaliza
career yake ya boxing Mayweather alimchagua Andre Berto kucheza nae
pambano la mwisho ambalo ni la 49. Kama ilivyotegemewa na wengi kwamba
lazima Berto angechezea kichapo basi imekua hivyo hivyo na Mayweather
amefikia 49-0 na kumaliza career yake bila kupigwa na boxer
yoyote.Japokuwa watu bado hawajafurahia michezo 49, wanasisitiza
kumaliza kwa michezo 50 ndio rekodi nzuri. Mayweather mwenyewe
anaendelea kusisitiza kwamba huu ndio mchezo wake wa mwisho kwenye
boxing.Karatasi ya takwimu za mchezo huo umeonyesha jinsi gani
Mayweather amecheza vizuri na kushinda bil ubishi.
0 comments