HISPANIA YAWEKA REKODI MPYA ULAYA, YAINGIZA TIMU TANO MAKUNDI LIGI YA MABINGWA
HISPANI
imeweka rekodi ya kuwa nchi ya kwanza kuingiza timu tano katika hatua
ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya Valencia kuitoa Monaco ya
Ufaransa kwa jumla ya mabao 4-3 katika mechi za mchujo usiku wa jana.
Los
Che, waliokuwa washindi wa pili kwenye michuano hiyo mwaka 2000 na
2001, wanaungana na vinara wengine wa La Liga walioshika nafasi tatu za
juu, Barcelona, Real Madrid na Atletico Madrid, wakati Sevilla
waliomaliza nafasi ya tano nao pia wamefuzu baada ya kutwaa taji la
Europa League mapema mwaka huu.
Bao
la ugenini la mshambuliaji wa zamani wa Manchester City, Alvaro Negredo
ndilo lililoibeba Valencia mjini Monacon jana ikifungwa 2-1. Negredo
alianza kufunga dakika ya nne kabla ya Andrea Raggi kuwasawazishia
wenyeji dakika ya 17 na Elderson Echiejile kufunga la pili dakika ya 75.
Category: uingereza
0 comments