Mdudu wa sare atawala Ligi Kuu Tanzania Bara
* Simba yabanwa Kaitaba, Ashanti yaikomalia Mbeya City
| Mbeya City iliyobanwa na Ashanti United |
| Kagera Sugar iliyoibana Simba uwanja wa Kaitaba |
| Simba |
| Ashanti United |
WAKATI klabu ya
Mbeya City ikibanwa jijini Dar es salaam na Ashanti United kwa kutoka
sare ya kutofungana, mdudu wa sare aliibukia pia uwanja wa Kaitaba
wakati kagera Sugar na Simba zilipofungana 1-1.
Mbeya City iliyokuwa ikipewa nafasi ya
kuiengua Yanga kwenye nafasi ya pili japo kwa muda, ilishindwa
kufurukuta kwa watoto wa mjini na kuambulia pointi moja iliyowafanya
wafikishe pointi 46.
Pointi hizo ni sawa na za Yanga ambayo
kesho inatarajiwa kushuka dimbani kucheza na JKT Ruvu katika pambano
linalosubiriwa kwa hamu litakalochezwa uwanja wa Taifa.
Mjini Bukoba, wenyeji Kagera Sugar
ilishindwa kufurukuta nyumbani baada ya kulazimishwa sare ya bao 1-1,
wenyewe wakilazimika kusawazisha bao la Simba lililofungwa na Zahor Pazi
katika dakika ya 45.
Bao hilo la kuwasawazisha, liliwekwa
kimiani na Themi Felix 'Mnyama' katika kipindi dakika ya 61 na kuifanya
timu yake kugawana pointi na Simba na kuendelea kusaliwa katika nafasi
ya nne na tano.
Ligi hiyo inatarajiwa kuendelea kesho kwa
mechi nne katika viwanja mbalimbali Coastal Union kuumana na Mgambo JKT
kwenye uwanja wa Mkwakwani, Yanga kuumana na JKT Ruvu uwanja wa Taifa,
Oljoro JKT itapepetana na Prisons ya Mbeya na Rhino Rangers
itaikaribisha Mtibwa Sugar mjini Tabora, mecchi ya Azam na Ruvu Shooting
imesogezwa mbele hadi Jumatano.
Category: tanzania


0 comments