Manchester City yaua England
![]() |
Edin Dzeko (10) akiifungia City bao la tatu |
MANCHESTER City
imeendelea kuonyesha dhamira yake ya kunyakua taji la Ligi Kuu England,
baada ya mapema leo kuifumua bila huruma Southampton kwa kuicharaza
mabao 4-1.
Bao la dakika tatu lililofungwa na
Mwanasoka Bora wa Afrika, Yaya Youre kwa mkwaju wa penati, liliwashtusha
wageni kabla ya kulirejesha dakika ya 37 kupitia Rickie Lambert pia kwa
penati.
Samir Nasir aliiongezea Man City bao dakika
ya 40 kwa pasi ya David Siliva na dakika nne ya nyongeza Edin Dzeko
alifunga bao la tatu akimalizia kazi nzuri ya Kolarov.
Bao lililowewanyong'onyesha Southampton lilizalimishwa kwenye dakika ya 81 na Jovetić akimalizia kazi ya Jesus Navaz.
Category: uingereza
0 comments