Emmanuel Okwi azungumza kuhusu taarifa za kuondoka Yanga, hiki ndicho alichosema

Unknown | 11:25 PM | 0 comments



OKWI
Siku kadhaa baada ya kutoka taarifa kwamba mshambuliaji wa kimataifa wa Uganda anayekipiga klabu bingwa ya Tanzania bara Yanga, Emmanuel Okwi amegoma kuendelea kuichezea timu hiyo kutokana na kuidai timu hiyo, hatimaye leo hii kupitia ukurasa wake wa mtandao wa Facebook Okwi amevunja ukimya na kuzungumzia suala hilo.

Hiki ndicho alichoandika leo

OKWI copy


Kwa mujibu wa Okwi sio kweli kwamba ameondoka Yanga, bali amepata majeraha ya goti yanayomfanya asiwepo kwenye kikosi cha Yanga. Amewashukuru mashabiki wa klabu hiyo kwa imani waliyonayo juu yake na kuahidi kurudi dimbani kuitumikia klabu hiyo atakapopona.

Share story hii kupitia>>>>>> :
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

Category:

0 comments