MAMBO UNAYOTAKIWA KUYAFAHAMU KUELEKEA UCL

Unknown | 4:44 PM | 0 comments

Jumla ya vilabu 22 vimefanikiwa kutwaa taji la Ulaya tangu kuanzishwa kwake mwaka 1955, huku Real Madrid ikiwa klabu pekee kutwaa taji hilo mara 10 pamoja na kutwaa mara tano mfululizo katika miaka mitano ya mwanzo.

Kuna vilabu vingine viwili pekee ambavyo vimefanikiwa kufika fainali mara 10, Milan na Bayern Munich. Jumla ya klabu 12 zimefanikiwa kushinda taji hilo mara mbili, miongoni mwa hivyo ni pamoja na vitatu ambavyo vimeorodheshwa hapo juu pamoja na Liverpool, Ajax, Barcelona, Internazionale, Manchester United, Benfica, Nottingham Forest, Juventus na Porto. Jumla ya vilabu 17 vimewahi kufika hatua ya fainali lakini havikuwahi kushinda taji hilo

Vilabu kutoka mataifa 10 tofauti vimetoa washindi wa kombe hilo. Hispania inaongoza kwa kutoa vilabu vilivyowahi kushinda taji hilo, vilabu vya Hispania vimelitwaa kombe hilo mara 15. Italy na England wanafungana kwa vilabu vyao kulichukua kombe hilo mara 12 wakifuatiwa na Ujerumani ambayo imetoa washindi mara saba, vilabu vya Uholanzi vimebeba mara sita huku Ureno wakiwa wametoa washindi mara nne. Mataifa mengine yakiwa yakiwa yametoa washindi mara moja tu, Scotland, Romania, Yugoslavia na Ufaransa wakati Greece, Belgium na Sweden zikiwa hazijawahi kutoa washindi badala yake vilabu vyao vimewahi kufungwa kwenye mechi za fainali.

Klabu kutoka katika majiji 35 ya Ulaya zimeshiriki fainali ya mashindano hayo huku majiji 21 yakitoa washindi. Madrid na Milan wakitoa washindi mara 10. AC Milan na Inter Milan wamelitoa kimasomaso jili la Milan wakati Real Madrid pekee ndiyo imeshinda taji hilo kutoka jiji la Madrid huku Atletico Madrid ikipoteza mechi zake mbili za fainali.

Miji na majiji yaliyowahi kutoa mabingwa wa European Cup/UEFA Champions League


Share story hii kupitia>>>>>> :
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

Category:

0 comments