AZAM YAIPIGA VIWILI MAJIMAJI

Unknown | 7:46 PM | 0 comments


AZAM FC imeipiga kumbo Simba SC katika mbio za ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kufuatia ushindi wa mabao 2-0 jioni ya leo dhidi ya Majimaji ya SOngea Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.
Shujaa wa Azam FC leo alikuwa ni kiungo Mudathir Yahya Abbas aliyefunga mabao yote mawili kipindi cha pili, dakika ya 51 na 63.


Azam FC sasa pointi 58 baada ya kucheza mechi 25 za Ligi Kuu na kupanda hadi nafasi ya pili, nyuma ya mabingwa watetezi, Yanga yenye pointi 62 za mechi 25 pia, ikiiteremshia Simba yenye pointi 57 za mechi 25 pia nafasi ya tatu. BIN ZUBERY
Kikosi cha Azam FC leo kilikuwa; 28 Aishi Manula, Erasto Nyoni, Gadiel Michael/ Abdallah Kheri dk71, David Mwantika, Aggrey Morris, Jean Mugiraneza, Ramadhan Singano ‘Messi’, Mudathir Yahya, Salum Abubakar ‘Sure Boy’, Didier Kavumbagu/Ame Ali ‘Zungu’ k46 na Khamis Mcha/ Shaaban Iddi dk84.

Share story hii kupitia>>>>>> :
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

Category:

0 comments