MATOKEO KAMILI YA MECHI ZOTE ZA LEO NOV 28 ZA LIGI KUU YA UINGEREZA HAYA HAPA ...

Unknown | 11:23 PM | 0 comments




November 28 mtu wangu wa nguvu unayependa soka la Ulaya hususani Ligi Kuu Uingereza, ninazo headlines Za matokeo ya mechi za leo November 28, Ligi Kuu Uingereza November 28 imepigwa michezo sita ya muendelezo wa Ligi hiyo kwani ni mechi ambazo zitafanya kila timu iliyocheza leo kutimiza idadi ya mechi 14 kwa msimu wa 2015/2016.
4381
Miongoni mwa mechi zilizochezwa November 28 ni mechi kati ya Leicester City dhidi ya Manchester United, mchezo uliyopigwa katika dimba la King Power Stadium, mchezo huo ambao unatajwa kuhudhuriwa na watu zaidi ya  30000, ulikuwa mgumu kidogo kwa Man United kwani dakika ya 24 Jamie Vardy alianza kupachika goli la kuongoza kwa Leicester City goli la kwanza.
4305
Man United walipata nafasi ya kusawazisha goli dakika ya 45 kupitia kwa kiungo wake wa kimataifa wa Ujerumani Bastian Schweinsteiger, licha ya kuwa Man United walionesha jitihada za kutaka kupata ushindi ili waweze kufikisha point 30 na kukaa kileleni mwa msimamo wa Ligi Uingereza, mchezo ulimalizika kwa sare ya goli 1-1.
3824
Matokeo ya mechi nyingine za Ligi Kuu Uingereza zilizochezwa November 28
  • AFC Bournemouth 3 – 3 Everton
  • Aston Villa 2 – 3 Watford
  • Crystal Palace 5 – 1 Newcastle United
  • Manchester City 3 – 1 Southampton
  • Sunderland 2 – 0 Stoke City
  • Leicester City 1 – 1 Manchester United

Share story hii kupitia>>>>>> :
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

Category:

0 comments