Hiki ndicho kilichomtokea Neymar baada ya kumkabidhi refa zawadi ya jezi yake
Kuna mengi katika mchezo wa soka
tumewahi kuyashuhudia mtu wangu lakini imezoeleka katika maisha ya
kawaida kwa wachezaji, mfano ni kawaida kwa wachezaji soka kubadilishana
jezi baada ya mchezo na kuna wakati Mbwana Samatta wa Tanzania aliomba kubadilishana jezi na Ahmed Musa anayekipiga CSK Moscow ya Urusi kama ishara ya kumbukumbu ya ukarimu wa Musa wakati wa majaribio yake CSK Moscow, tukio hilo lilitokea wakati Taifa Stars ilipokutana na Nigeria uwanja wa Taifa Dar Es Salaam.
Mshambuliaji wa kimataifa wa Brazil Neymar ameingia katika headlines baada ya kumalizika kwa mchezo kati ya timu yake ya taifa ya Brazil dhidi ya Peru, mchezo wa kuwania kufuzu Kombe la Dunia 2018 Urusi lakini Brazil iliibuka na ushindi wa goli 3-0 magoli ambayo yalifungwa na Douglas Costa, Renato Augusto, na Felipe Luis.
Baada ya mechi kumalizika Neymar aliona ni vyema kwenda kumpa zawadi ya jezi muamuzi wa mechi hiyo Jose Buitrago kutokea Colombia lakini muamuzi aliikataa jezi ya Neymar
kitendo ambacho kinatafsirika kama muamuzi huyo aliogopa kuchukua kwa
sababu huenda angeonekana kapendelea, lakini utamaduni wa kupata saini
au jezi ya staa kwa watu wa nje ya Afrika ni kitu muhimu sana na wanaheshimu hivyo wengi walishangazwa kuona kapotezea kumbukumbu muhimu.
Category: uingereza
0 comments