Hii ni Top 10 ya wachezaji wabunifu zaidi katika Ligi Kuu Uingereza .... adui wa Taifa Stars ndani …
November 18 nimekutana na list ya wachezaji wabunifu zaidi katika Ligi Kuu Uingereza ila Top 10 hii iliyoandikwa na mtandao wa teamtalk.com
imetaja majina ya wachezaji 10 yanayotajwa kuwa na ubunifu uwanjani
kutokana na uwezo wao wa kutoa pasi za mwisho katika ufungaji wa magoli.
List hii inaongozwa na kiungo wa kimataifa wa Ujerumani anayekipiga katika klabu ya Arsenal Mesut Ozil.
1- Mesut Ozil ana rekodi ya kuwa mchezaji anayeongoza kwa kutoa pasi za mwisho kwa Cristiano Ronaldo na kufunga wakati yupo Real Madrid. Ozil anatajwa kuwa na rekodi ya kutoa pasi za mwisho (assist) 10 katika mechi 11. Kwa ujumla Ozil anatajwa kutengeneza nafasi za magoli 54 ambapo ni wastani wa 4.9 kwa mechi moja.
2- Dimitri Payet anakipiga katika klabu ya West Ham United anatajwa kuwa na assist tatu tu nyuma ya Ozil ila Dimitri Payet anatajwa kutengeneza wastani wa nafasi 3.9 kwa mechi moja, hii inamuweka katika list hii.
3- Christian Eriksen uwezo wa Eric Dier ana Dele Alli umekuwa ukionekana sana uwanjani kutokana na mchango wa Christian Eriksen , Eriksen anatajwa kuwa na rekodi ya kutengeneza wastani wa nafasi 3.1 kwa mechi.
4- Dusan Tadic
ana rekodi nzuri pia na yakuvutia anatajwa kupiga wastani wa pasi 26.5
kwa mechi lakini pia amemudu kutengeneza jumla ya nafasi tatu kwa mchezo
mmoja.
5- Kevin De Bruyne ana miezi michache toka arudi katika Ligi Kuu Uingereza
kwa mara nyingine tena ila anaonekana kufanya vizuri katika Top 10
anatajwa kuwa na assist nne katika mechi saba alizoanza na moja akitokea
benchi huyu ana wastani wa 3.0 ya utengenezaji wa nafasi za magoli
uwanjani.
6- Santi Cazorla anacheza pamoja na Francis Coquelin katika kikosi cha Arsenal,
ametengeneza wastani wa nafasi 2.9 katika mechi 12 na assist 3, lakini
pia anatajwa kuwa na ratio ya 90.6% ya kupiga pasi zilizokamilika yaani
bila kuharibiwa na adui.
7- Eden Hazard wachezaji wengi wa Chelsea msimu huu wanatajwa kufanya vibaya uwanjani ispokuwa Eden Hazard
anaonekana kuendelea kufanya vizuri uwanjani na bado yupo nafasi ya
saba kwa kutengeneza nafasi za magoli kwa kuwa na wastani wa 2.7.
8- James Milner katika nafasi ya nane ametengeneza wastani wa nafasi 2.5 kwa mechi lakini anatajwa kuwa na assist tatu, hata hivyo ujio wa Jurgen Klopp unatajwa kumfanya mchezaji huyo kuongeza wastani wake wa kufanya vizuri uwanjani.
9- Erik Lamela
anatajwa kutengeneza wastani wa nafasi 2.4 hadi sasa na anatajwa kuanza
jumla ya mechi nane na kufanya assist 3. Lakini ameingia mechi tatu
akitokea benchi nje ya mechi nane alizoanza.
10- Riyad Mahrez huyu anafunga Top 10 ya wachezaji wabunifu katika Ligi Kuu Uingereza lakini ni miongoni mwa wachezaji wa Algeria walioifunga Taifa Stars magoli 7-0, Riyad Mahrez akipachika goli la tatu dakika ya 43. Riyad Mahrez pia amefungana na Moussa Sissoko na Nathan Redmond katika Top 10 kwani wote wanawastani wa 2.2 kwa mechi.
Category: uingereza
0 comments