Huyu ndiye kiongozi mpya wa FIFA!!

Unknown | 9:39 PM | 0 comments

 



Masaa machache baada ya Rais wa FIFA Sepp Blatter kusimamishwa kuliongoza shirikisho hilo, kiongozi wa shirikisho la soka Afrika Issa Hayatou kutoka Cameroon amepewa jukumu la kuongoza shirikisho hilo kwa muda.
Hayatou atachukua nafasi hiyo kufuatia kusimamishwa kazi kwa Rais huyo wa FIFA kwa muda wa siku 90 na Kamati ya Maadili ya shirikisho hilo.
Hayatou, ambaye aliongoza CAF tangu mwaka 1988, pia alikuwa makamu wa rais katika kamati ya utendaji ya Fifa aliyehudumu muda mrefu zaidi.
PLATIN
Sepp Blatter na Michel Platini wote wamesimamishwa kazi
Blatter amesimamishwa kwa muda wa siku 90 kufuatia kashfa mpya ambayo imeibuka hivi karibuni ndani ya shirikisho hilo ikihusisha malipo ya fedha ambazo ziliandikishwa kwa akaunti ya rais wa shirikisho la vyama vya soka barani Ulaya Michel Platini
Rais mpya wa FIFA atapatikana Februari 26, 2016.

Share story hii kupitia>>>>>> :
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

Category:

0 comments