Blatter wa FIFA asimamishwa kazi

Unknown | 9:09 PM | 0 comments


Shirikisho la soka duniani Fifa limemsimamisha kazi kwa mda rais wake Sepp Blatter ,katibu wake Jerome Valcke na makamu wa rais Michel Platini kwa siku tisini.



Aliyekuwa makamu wa rais wa shirikisho hilo Chung Mong-joon pia naye amepigwa marufuku kwa miaka sita mbali na kutozwa faini ya Faranga za Uswizi 100,000.
Adhabu hiyo ilitolewa na kamati ya maadili katika shirikisho hilo.
Blatter,Valcke na rais wa UEFA Platini wanachunguzwa na kamati hiyo kuhusu madai ya ufisadi.
Taarifa zinasema kuwa Uamuzi huo unatokana na uchunguzi unaofanywa na kamati ya maadili katika shirikisho hilo
Watatu hao wamepigwa marufuku kushiriki katika michezo yoyote ya kandanda kwa mda huo.Wamekana madai ya kufanya uovu wowote.Kamati hiyo ilianza kumchunguza bwana Blatter baada ya jaji mkuu wa Uswizi kufungua mashtaka dhidi ya rais huyo mwenye umri wa miaka 79.
Anatuhumiwa kwa kutia saini kandarasi isiyokuwa na umuhimu wowote kwa FIFA mbali na kutoa malipo kwa rais wa shirikisho la UEFA Michel Platini kinyume na matakwa ya shirikisho hilo.
Platini pia amesimamishwa kazi.
Kamati ya maadili pia ilianzisha uchunguzi dhidi ya Platini kuhusu malipo hayo ya Yuro milioni 2 ambayo yalifanywa miaka minane baada ya PLatini kumfanyia kazi Blatter.
Valcke tayari alikuwa katika likizo kufuatia taarifa ilioandikwa katika gazeti moja kwamba anahusika na kashfa ya kutaka kujinufaisha na tiketi za kombe la dunia.

Share story hii kupitia>>>>>> :
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

Category:

0 comments