MANCHESTER UNITED 2-1 EVERTON, CHELSEA 2-0 ARSENAL

Unknown | 9:33 AM | 0 comments


Na Sultani Kipingo
Yaani ni kama kwamba kubadilika kimchezo kwa kipa wa Man U David de Gea kutoka kuwa mchekea hadi mmoja wa makipa bora wa ligi kuu ya Uingereza kumekamilika. De Gea, hapana shaka, leo amedhihirisha kuwa mmoja wa walinda mlango hodari, tofauti na na msimu uliopita alipookuwa chini ya kocha David Moyes. Leo Mhispania huyu ameokoa penati na kupangua mipira kibao kumyima Mzee Arsene Wenge na Arsenal
yake pointi 2 na kumuokoa kocha mpya Louis van Gaal kutoka katika kuti kavu
Ngoma ilikuwa nzito toka kipyenga cha kwanza. Ulikuja pale Cesc Fabregas alipotoa pande tamu kwa Diego Costa ambae alipiga bao moja tamu sana. Kofi la uso kwa mashabiki walioanza kumbeza. Hata hivyo jambo ambalo lingempa hofu Wenger na timu zote zingine ni kwamba leo Chelsea wametandaza kabumbu lisilo la kawaida, na kuhakikisha kuwaNhio sio timu ya mtu mmoja. Naam, Costa alifunga tena, lakini hakuwa akihitajika sana. Maana ngoma aliyopiga Eden Hazard si ya kawaida kiasi hata Costa asingefunga, bado tu Chelsea wangepata mabao kwa njia zingine.

Share story hii kupitia>>>>>> :
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

Category:

0 comments