NOOIJ ATANGAZA KIKOSI CHA STARS KITAKACHOIVAA MSUMBIJI

Unknown | 6:55 AM | 0 comments

Kocha wa Timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars, Martinus Ignatius "Mart" Nooij akitangaza kikosi cha wachezaji 20 watakaoivaa timu ya Taifa ya Msumbiji ‘Mambas’.
Wachezaji wa Stars wanaocheza soka la kulipwa nje ya nchi Mwinyi Kazimoto (kulia) wa Al Markhiya ya Qatar na Thomas Ulimwengu (TP Mazembe ya DR Congo wakimsikiliza kocha Nooij akitaja kikosi.
Na Mohammed Mdose
KOCHA mkuu wa timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ ametangaza kikosi cha wachezaji 20 watakaoivaa timu ya Taifa ya Msumbiji ‘Mambas’ kwenye mchezo wa kusaka tiketi ya kufuzu fainali za mataifa huru ya Afrika (AFCON) zinazotarajiwa kufanyika mwakani nchini Morooco unaotarajiwa kupigwa Jumapili kwenye dimba la Taifa jijini Dar.
Kwenye kikosi hicho Nooij amewajumuisha Thomas Ulimwengu, Mwinyi Kazimoto na Mbwana Samatta ambao wanacheza soka la kulipwa nje ya nchi.

Wachezaji wanaounda kikosi hicho ni:
Makipa- Deogratius Munish ‘Dida’ (Yanga) na Aish Manula (Azam).
Mabeki-Shomari Kapombe, said Morad na Erasto Nyoni (Azam), Oscar Joshua, Kelvin Yondan na Nadir Haroub ‘Canavaro’ (Yanga), Edward Charles (JKT Ruvu).

Viungo-Mwinyi Kazimoto (Al Markhiya), Himid Mao (Azam), Mrisho Ngasa (Yanga), Haruna Chanongo, Ramadhani Singano ‘Messi’ na Amri Kiemba (Simba).
Washambuliaji-Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu (TP Mazembe), John Bocco (Azam), Simon Msuva (Yanga) na Mcha Hamis (Azam).
Kama Stars itafanikiwa kuitupa nje Mambas itatinga moja kwa moja kwenye hatua ya makundi ambapo itaungana na timu za Niger, cape Verde na Zambia.Viingilio kwenye mchezo huo.

Wakati huo huo mchezaji Thomas Ulimwengu amewataka Watanzania kutegemea makubwa katika mchezo huo Ulimwengu ambae amepachikwa jina la Rambo na mashabiki wa klabu ya TP mazembe amesema anaimani kubwa kuwa timu imejiandaa vizuri chini ya kocha Nooij ili kuhakikisha wanawasukuma nje Manbas na kutinga hatua ya makundi.

Alisema kuwa anaamini katika hilo kwani wachezaji wenzake wapo fit kisaikolojia na kimwili na pia kutokana na kocha wa Stars kuwahi kuifundisha timu ya Msumbiji yanazidi kuwatia moyo na ari ya kuamini watapambana kuhakikisha wanaibuka kifua mbele. “Tunaahidi makubwa katika mechi hiyo, tumejipanga vizuri kwa hilo kikubwa Watanzania watusapoti na waje kwa wingi,” alisema Ulimwengu.

Viingilio vya mchezo huo vilivyotangazwa na Shirikisho la Soka Nchini (TFF) ni kiwacngo cha chini ni shilingi 7000, 30,000 na viti maalumu (VIP) shilingi 45,000.
Ofisa habari wa shirikisho la soka Tanzania Bonface Wambura amesema kuwa kuanzia kesho asubuhi tiketi za kieletronic zitauzwa kwenye magari maalumu kwenye vituo vya Buguruni Shelly,Dar live Mbagala, Ferry Magogoni, kigamboni, oil com Ubungo, oil com Chang’ombe shule ya sekondari Benjamini Mkapa (kariakoo), TCC club chang’ombe na uwanja wa Taifa.

“Tiketi zinapatikana kupitia M-PESA kwa kupiga *150*00# kisha bonyeza 4, bonyeza tena 4 kisha weka namba ya kampuni 173399 kisha ingiza 7000 kama namba ya kumbukumbu ya malipo, kisha andika tena 7000 kwenye weka kiasi, kasha weka namba ya siri na baadaye bonyeza 1 kukubali,”alisema Wambura.


GPL

Share story hii kupitia>>>>>> :
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

Category:

0 comments