Home �
tanzania
� HUZUNI! MBEYA CITY FC YACHAPWA 1-0 NA VICTORIA UNIVERSITY ROBO FAINALI
Unknown |
10:33 AM |
0
comments
Na Baraka Mpenja, Dar es salaam
WAWAKILISHI wa Tanzania katika michuano ya CECAFA Nile Basin
Cup, Mbeya City fc wameaga mashindano hayo baada ya kufungwa bao 1-0
dhidi ya Victoria University ya Uganda katika mchezo wa robo fainali
uliomalizika dakika chache zilizopita mjini Khartoum.
Mbeya City wametolewa katika michuano hiyo wakiwa wameshinda
mechi moja, kufungwa moja na kutoka suluhu mechi moja katika hatua ya
makundi.
Lakini wamepoteza mechi ya pili katika mashindano haya baada ya kufungwa hatua ya robo fainali na kufungashiwa virago.
Afisa habari wa Mbeya City fc, Freddy Jackson amesema wanashukuru kwa kilichotokea kwani ndio matokeo ya mpira wa miguu.
Freddy amesema wachezaji wamejitahidi kucheza kwa juhudi, lakini hawakuwa na bahati.
“Ndugu tunashukuru kwa maombi yenu, alichotupangia mungu ndicho
tulichopata. Mechi imemalizika , Mbeya city O victoria 1, hivyo basi
tumeyaaga mashindano”. Amesema Freddy.
Share story hii kupitia>>>>>> :
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
Category:
tanzania
0 comments