BABA WA SERGIO AGUERO ADAI MTOTO WAKE ANAPENDA KWENDA BARCELONA
BABA
mzazi wa Sergio Aguero ameweka wazi kuwa mshambuliaji huyo wa
Manchester City anapenda kujiunga na Barcelona na vyombo vya habari
nchini Hispania vimeripoti kuwa wababe hao wa Katalunya wanajiandaa
kuweka mezani ofa ya paundi milioni 31.
Barcelona
wapo tayari kufikia paundi milioni 47 ili kuinasa saini ya nyota huyo
wa kimataifa wa Argentina kama Man City watakataa ofa yao ya kwanza.
Lakini
kocha mpya wa Barcelona, Luis Enrique ameripotiwa kuvutiwa zaidi na
Aguero na yuko tayari kumwaga kitita kirefu cha fedha kama Man City
watakataa., hii ni kutokana na mtandao wa michezo wa Hispania.


Aguero
mwenye miaka 25, ana uhusiano mzuri na nyota wa Barcelona, Lionel Messi
na Enrique anaamini kuwa kuwaweka pamoja kunaweza kuisaidia klabu na
Argentina kwa ujumla.
Mkataba
wa Aguero utamalizika mwaka 2017, lakini klabu yake inaweza kumuuza
zaidi ya paundi milioni 36 walizotumia kumsajili mwaka 2011.
Aguero
alikuwa na msimu mzuri Etihad licha ya kuwa na majeruhi. Alifunga
magoli 28 na kuwasaidia Man City kubeba kombe la ligi kuu na Capital
One.
Category: uingereza
0 comments