LIVERPOOL RAHA MPAKA BASI, PENALTI MBILI ZA GERARD ZAFANYA KILELENI YAWE MAKAZI YAO YA KUDUMU
MABAO
mawili ya penalti ya Steven Gerrard yameipa ushindi wa 2-1 Liverpool na
kuweka hai matumaini ya ubingwa wa Ligi Kuu ya England.
Lakini
timu zote, West Ham na Liverpool ziliondoka uwanjani zimemkasirikia
refa Anthony Taylor kwa kuvurnda katika maamuzi yake kwenye mchezo huo
ambayo yaliiponza timu kufungwa bao.
West
Ham walilalaimia penalti iliyotolewa kabla ya mapumziko baada ya James
Tomkins kuunawa mpira na Gerrard akafunga dakika ya 44. Lakini wachezani
wa Liverpool walilalamikia pia bao la kusawazisha la West Ham lililofungwa Guy Demel dakika ya 45.
Mshambuliaji
wa zamani wa Wekundu hao wa Anfiled, Andy Carroll alimchezea rafu ya
wazi na kipa Simon Mignolet wakati wa mpira wa kona, akimpiga kichwani
na kusababisha Mbelgiji huyo mpira umponyoke na kuangukia kwa Guy Demel,
aliyefunga akiwa anatazamana na nyavu.
Liverpool
ilipata bao la pili kwa penalti ya utata, baada ya kipa wa West Ham,
Adrian kudaiwa amemchezea rafu Jon Flanagan, lakini picha za marudio ya
Televisheni zilimuonyesha mlinda mlando huyo akiufikia mpira kwanza na Gerrard akaenda kufunga.
Ushindi
huo unaifanya Liverpool ifikishe pointi 74 baada ya kucheza mechi 33 na
kuendelea kula raha kileleni mwa Ligi Kuu ya England, mbele ya Chelsea
yenye pointi 72 za mechi 33 na Manchester City yenye pointi 70 za mechi
31.
Haijalishi, sisi ubingwa tu: Steven Gerrard akisherehekea na wenzake baada ya kufunga penalti iliyoipa bao la ushindi Liverpool
Category: uingereza



0 comments