PELLEGRINI AWA KOCHA BORA TENA LIGI KUU ENGLAND,ADAM JOHONSON NDIYE MCHEZAJI MKALI KULIKO WOTE
KOCHA
Manuel Pellegrini ameshina tuzo ya kocha bora wa mwezi Ligi Kuu ya
England, baada ya Manchester City kuweka rekodi nzuri Januari ikishinda
mechi nne kati ya nne.
Huu
ni mwezi wa pili mfululizo Pellegrini anashinda tuzo hiyo - na mara ya
kwanza kwa kocha mmoja kushinda mara mbili mfululizo tangu Carlo
Ancelotti afanye hivyo akiwa kocha wa Chelsea mwaka 2011.
Nyota
wa Sunderland, Adam Johnson ameshinda tuzo ya mchezaji bora wa mwezi wa
Ligi Kuu baada ya kazi nzuri aliyoifanya mwezi uliopita akifunga mabao
matano.
Mfululizo: Kocha wa Manchester City, Manuel Pellegrini ameshinda tuzo ya kocha bora wa mwezi wa Ligi Kuu England

Kiboko yao: Nyota wa Sunderland, Adam Johnson ameshinda mchezaji bora wa mwezi
Category: uingereza
0 comments