NDOA YAMUONDOA MKWASA UTURUKI, ALAZIMIKA KURUDI DAR
MKWASA (KULIA) AKIWA UTURUKI NA ROBERTO CARLOS NA KIUNGO WAKE NIZAR KHALFAN |
Kocha
Msaidizi wa Yanga, Charles Boniface Mkwasa analazimika kurejea nyumbani jijini
Dar es Salaam na kuiacha Yanga ikiendelea na mazoezi mjini Antalya, Uturuki.
Mkwasa
ambaye amesafiri na Yanga iliyoweka kambi nchini humo atatua nchini Ijumaa ili
kushughulikia masuala yanayohusiana na ndoa yake.
Hata hivyo Mkwasa atalazimika kusubiri hadi Kocha Mkuu mpya, Hans van Der Pluijm ajiunge na kikosi hicho.
Yanga
inaingia naye mkataba wa miaka miwili na ataondoka keshokutwa Jumanne
kwenda Uturuki wakati kesho anataka kwenda Zanzibar kuiona Simba ya
Zdravko Logarusic ikicheza fainali ya Kombe la Mapinduzi.
Mkwasa ni
mme wa Mkuu wa Wilaya wa Bahi, Betty Mkwasa na kurudi kwake ni kwa ajili ya
sherehe yao ya kusherekea zaidi ya miaka 20 ya ndoa yao.
Mkwasa amejiunga
na Yanga akitokea Ruvu Shooting alikokuwa kocha mkuu na sasa anaitumikia Yanga
katika nafasi ya kocha msaidizi.
Taarifa za
uhakika kutoka ndani ya Yanga zinaeleza, uongozi umelazimika kumpa Mkwasa
ruhusa hiyo kwa kuwa alikuwa na mipango hata kabla ya kuajiliwa.
“Mkwasa
alikuwa mkweli kabla ya kuajiliwa, ilikuwa ni uongozi uangalie suala hilo maana
aliliweka mezani mapema na lazima asherekee.
“Kwa hiyo
uongozi ukakubali, kikosi kizima kitarejea nchini Januari 22, lakini Mkwasa
analazimika kurudi mapema, nafikiri ni Januari 17,” kilieleza chanzo cha
uhakika.
Tayari
Mkwasa ameiongoza Yanga kushinda mechi ya kwanza ya kirafiki kwa mabao 3-0,
mechi hiyo ilipigwa juzi katikia Uwanja wa Hoteli ya Sueno Beach Side nje
kidogo ya mji wa Antalya.
Category: tanzania
0 comments