MAN CITY YAREJEA KILELENI LIGI KUU ENGLAND, MWAKA HUU KAZI IPO
MABAO
ya Edin Dzeko na Alvaro Negredo yametosha kuipa ushindi wa 2-0
Manchester City dhidi ya Newcastle Uwanja wa St James Park na kurejea
kileleni mwa Ligi Kuu England.
Nyota wa Bosnia alifunga bao la kwanza dakika ya nane akiunganisha krosi ya Aleksandar Kolarov kumtungua kipa Tim Krul.
Kikosi
cha Alan Pardew kilidhani kimepata bao la kusawazisha baada ya shuti la
mbali la Cheick Tiote kumpita kipa Joe Hart na kutinga nyavuni, lakini
likakataliwa kwa sababu Yoan Gouffran alikuwa ameotea.
Negredo
akaifungia City bao la pili dakika za majeruhi. Ushindi huo unaifanya
City irejee kileleni baada ya kutimiza pointi 47 kutokana na mechi 21,
ikiishusha Chelsea yenye pointi 46 baada ya kucheza mechi 21 pia katika
nafasi ya pili. Arsenal sasa ni ya tatu kwa pointi zake 45, ingawa
imecheza mechi 20.
Kazi
nzuri: Mshambuliaji wa Manchester City, Edin Dzeko (kulia) akimtungua
kipa wa Newcastle, Tim Krul kuifungia bao la kwanza timu yake
Krul (kulia) hakuweza kuuzuia mchomo wa Dzeko
Dzeko akikimbia kushangilia baada ya kufunga
Anapongezwa na wenzake
Category: uingereza
0 comments