WAHUSIKA WAWAJIBIKE KUTEGUA KITENDALIWI CHA OKWI KWA MASHABIKI WA SIMBA…MWANASHERIA NDUMBARO AFUMUA UKWELI!!
Na Baraka Mpenja wa Fullshangwe, Dar es salaam
Tel: 0712461976 au 0764302956
SIKU
kadhaa baada ya Yanga kutangaza kumsajili mchezaji hatari kutoka SC
Villa ya Uganda, Emmanuel Anord Okwi, wanachama wa klabu ya Simba sc na
wadau wa michezo wameshindwa kutegua kitendawili cha nani mmiliki wa
mchezaji huyo kati ya Etoile Du Sahel ya Tunisia na SC Villa ya Uganda.
Wakati
wote wamekuwa wakipiga simu na kutuma ujumbe mfupi wa simu wakihitaji
ufafanuzi juu ya sakata hili ambalo ndio habari ya mjini kwa sasa. Kila
kona ni usajili wa Okwi kwenda Yanga.
Yanga
wakati wanatangaza kumsajili okwi, mwenyekiti wa kamati ya mashindano
ya klabu hiyo, Abdallah Ahmed Bin Kleb alisema wamefuata tararibu zote
na kujiridhisha kuwa wapo sahihi kumsajili Okwi.
Bin
Kleb alienda mbali zaidi na kusema wamewaona wanasheria, wamefuatilia
hadi FIFA na kupata hati ya hukumu ya Okwi kushinda kesi dhidi ya klabu
yake ya Etoile ambayo alikuwa anadai haijamlipa mshahara wake kwa miezi
mitatu pamoja na baadhi ya hela za uhamisho wake.
“Tulimsajili
Okwi na mpaka sasa tumepata Hati yake ya Uhamisho wa Kimataifa (ITC)
na ndio maana tumeweka mambo hadharani”. Alisema Bin Kleb siku
akitangaza usajili wa Okwi.
Okwi
aliuzwa na Simba kwenda klabu ya Etoile Du sahel ya Tunisia januari
mwaka huu kwa kitita cha dola 300, 000 za kimarekani, lakini hakudumu
katika klabu hiyo kwa madai ya kutolipwa haki zake na kuamua kurejea
kwao Uganda.
Okwi
baada ya kurejea kwao Uganda alikaa miezi sita bila kucheza na ndipo
shirikisho la kandanda la Uganda (FUFA) likasimama kidete kumpigania
aruhusiwe kureja nyumbani na kujiunga na Sport Club Villa ya Uganda
`Majogoo wa Kampala` ili kulinda kiwango chake.
Watu wamevurugwa: Okwi amewaacha hoi mashabiki wa Simba sc, hawaelewi nini kinaendelea, Yanga wachekelea usajili wake.
Okwi ni mchezaji wa Etoile inayodaiwa na Simba Sc kitita cha dola za kimarekani 300,000 na sakata hilo limefika mpaka FIFA.
Wakati
Yanga wakisema wamejiridhisha kumsajili Okwi na kuona wako sahihi,
Simba nao wanazungumza yao wakisema watani wao wa jadi wamejipalia mkaa
kwa usajili wa mchezaji huyo.
Mwenyikiti
wa kamati ya usajilli ya Simba, Kaptein Zacharia Hans Poppe alisema
Okwi ni mchezaji halali wa Etoile na kama Yanga wamemsajili bila
mawasiliano na klabu hiii na kudanganywa na Villa ambayo ilikuwa
inamtumia mchezaji kwa mkopo wa miezi sita tu, basi wameingia `shimo la
tewa.`.
Poppe
aliongeza kuwa shirikisho la soka nchini Uganda lilitaka kumtumia
mchezaji huyo kwenye fainali za mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa
ndani, lakini wakagonga mwamba baada ya kuambiwa haiwezekani kwani ni
mchezaji halali wa Etoile Du Sahel.
Yanga
wanajilinda zaidi na kueleza kuwa wameshafika FIFA na kupewa hati ya
hukumu ya kesi ya Okwi na klabu yake , ambapo Okwi kupitia kwa wakili
wake aliishitaki timu hiyo kwa kutomlipa fedha zake zikiwemo za
mshahara, baadaye alishinda na kuruhusiwa kuvunja mkataba wake.
Kuna
wakati iliwahi kuelezwa na Simba sc Kuwa Okwi aliruhusiwa na klabu yake
kwenda Uganda kuitumikia timu yake ya Taifa, lakini alichelewa kurejea
Tunisia na klabu ikampa adhabu ya kukatwa mishara ya miezi yoye ambayo
hakuwepo kazini.
Pia
alishushwa akafanye mazoezi na timu ya pili , lakini kama ilivyo kawaida
kwa Mganda huyo akapiga chini mpango na kuaanza kula bata tu mpaka
alipoamua kurejea kwao Uganda.
Hapa
ndipo mgogoro wa Etoile na Okwi ulipoanzia, lakini alipoenda kwao Uganda
alikuwa anakaa tu kwa miezi sita na ndipo FUFA wakaona ni busara
kumwombea ruhusa maalumu ya kucheza Villa ili kunusuru kiwango chake.
Amecheza
Villa kwa miezi kadhaa mpaka alipotangazwa kusajiliwa na Yanga desemba
15 mwaka huu zikiwa zimesalia saa chache kufunga dirisha dogo la
usajili.
Baada
ya kutoka kwa habari hii iliyogonga vichwa wa watu wengi, nimepokea
simu nyingi sana, kila mtu anataka ufafanuzi juu ya usajili huu
anaookena kuwa na utata.
Tatizo linaloonekana si Yanga imempataje mchezaji huyo?, watu wengi wanajiuliza nani ni mmiliki wa Okwi?.
Kama Etoile walimruhusu Okwi akacheze Villa kwa Mkopo halafu wamemuuza imekuwaje”
Je, kuna mazungumzo kati ya Villa na Etoile juu ya mchezaji huyu?. Pia Etoile wameilipa Simba fedha zake za mauzo?.
Yapo
maswali mengi yanayoulizwa na wasomaji juu ya usajili huu huku wakitaka
kujua Kama ni kweli Simba hawajalipwa fedha za Okwi. kama wamelipwa nani
kazipokea?. Kwanini Villa waruhusiwe kumuuza mchezaji ambaye yupo kwa
mkopo klabuni kwao tena kwa ruhusa maalumu ya FIFA?.
Kwa
sasa kuna mfumo wa Transfer Matching System (TMS). Kwa kutumia mfumo wa
Kisasa jina la mchezaji mwenye matatizo lisingeweza kukubali kuingia
katika orodha ya wachezaji wa Dar Young Africans.
Swali
la Msingi, imekuwaje Yanga wamefanikiwa kuliingiza jina la Okwi? Kwa
nini wamepata ITC kama kweli Okwi alikuwa ana matatizo?. FUFA wametoa
ITC wakijua Okwi ana matatizo?. Maswali ni mengi sana ambayo wadau wa
soka wanataka ufafanuzi.
Mtandao
huu ulikutana na mwanasheria ambaye ni wakala wa kimataifa wa
wachezaji, Dokta Damans Ndumbaro ambaye alifafanua kuwa ITC inatolewa na
shirikisho la nchi inayochezea kwa wakati husika.
Kwa tafsiri hiyo, Okwi alikuwa anachezea Uganda na ndio maana FUFA wametoa ITC.
Lakini Ndumbaro aliongeza kuwa FIFA hawatoi ITC, isipokuwa wanakuwa wanaangalia machakato mzima wa ITC ile.
Ndumbaro
aliongeza kuwa shirikisho la nchi husika linaweza kutoa ITC kwa
mchezaji hata kama ana matatizo, ila itategemeana na mazingira ya wakati
huu.
“Tatizo
la Okwi lipo Tunisia, kama SC Villa wameelewana na Etoile basi hakuna
tatizo. Lakini kama hawana mawasiliano na wao wamemuuza mchezaji
aliyekuwa kwa mkopo tu bila ridhaa yao, basi huo ni UTAPELI” na lazima
wawajibike kwa mujibu wa sheria. Alisisitiza Dkt. Ndumbaro.
Kama
nilivyosema awali, tatizo si Yanga kumsajili Okwi, tatizo lipo katika
mfumo uliotumika. Kuna watu wanawajibika kutegua kitendawili hiki.
Kama
kweli Okwi alishinda kesi FIFA, hakika Yanga wanatakiwa kutoa vielelezo
zaidi vinavyothitibisha uhalali wa wao kumsajili nyota huyo ikiwemo hiyo
hati ya hukumu waliyosema wanayo.
Anakwenda FIFA: Mwenyekiti wa Simba Sc, Ismail Aden Rage amesema anakwenda FIFA kuhusu suala la Okwi
Sheria
za FIFA ziko wazi kuwa klabu inatakiwa kuwa imemaliza kulipa malipo ya
fedha za kumnunua mchezaji kabla ya kumaliza Mkataba wake au kumtoa
sehemu nyingine, sasa Etoile watalazimika kuilipa Simba SC mara moja
kama walishindwa kesi na Okwi. Hakika Deni halifutiki, lazima dola
300,000 zilipwe kwa Simba sc.
Pia
tunatarajia TFF Kumaliza suala hili. Tunafahamu wanao mfumo mzuri wa
kumuidhinisha mchezaji kuichezea klabu husika, wadau wawe na subira
kidogo.
TFF
watawasiliana na FIFA na kupewa vielelezo vyota vya Okwi na uhalali wa
Yanga kumsajili, baada ya hapo wataamua kumuidhinisha kuitumia Yanga
kama wamefuata taratibu au kutoruhusiwa kuichezea klabu hiyo kama kuna
Matatizo.
Wengi wao wameduwaa tu, eti wahawaelewi suala la Okwi
Kwasasa
imekuwa ngumu kupata maelezo kutoka kwa Etoile Du Sahel juu ya sakata
lao na Okwi pamoja na Simba sc, lakini siku si nyingi ukweli
utafahamika.
Kwa
wale wanaoendelea kupiga simu na kunitumia ujumbe mfupi, hususani
mashabiki wa Simba sc, kikubwa ni wao kuwa watulivu, kwa mazingira
niliyosema hapo juu, dola zao 300,000 kama hazijaliwa zitalipwa tu,
lakini kama zilishalipwa hapo ni tatizo lingiine.
Mwenyekiti
wao Aden Rage tayari ameshasema uongozi umeandika barua kwenda FIFA
kuhusu madai yao ya dola 300,000 kwa klabu ya Etoile Du Sahel.
Kama kuna siasa ndani ya suala hili ni jukumu la wanachama kumhoji mwenyekiti wao ili kuondoa utata wa fedha za mauzo ya Okwi.
Sheria
zipo na siku zote huwa zinaweka mambo sawa.. Zipo wazi na zinaeleza
nini kifanyike, kwahiyo swala la usajili wa Okwi litatolewa ufumbuzi
kwani wahusika wapo kwa ajili ya kazi ya kutoa ufafanuzi juu ya nini
kimefanyika mpaka Yanga kumsajili.
Karibu sana kwa maoni na maswali
Baraka Mpenja
Tel: 0712461976
Category: tanzania
0 comments