TANZANITE YAWASILI JOHANNESBURG KUIVAA BATSESANA!!
Kikosi
cha wachezaji 20 na viongozi tisa cha timu ya Tanzania ya wasichana
chini ya miaka 20 (Tanzanite) kimewasili leo jijini Johannesburg tayari
kwa mechi dhidi ya wenyeji Afrika Kusini (Batsesana).
Mechi
hiyo ya marudiano ya raundi ya pili kuwania tiketi ya kucheza fainali
za Kombe la Dunia kwa wasichana wenye umri chini ya miaka 20
zitakazofanyika mwakani nchini Canada.
Tanzanite
imefikia Millpark Garden Court Hotel tayari kwa mechi hiyo
itakayochezwa Jumamosi katika Uwanja wa Dobsonville ulioko Soweto,
Johannesburg kuanzia saa 9.30 alasiri kwa saa za Afrika Kusini.
Wachezaji
wa Tanzanite walioko katika kikosi hicho ni Amina Bilali, Amina Hemed,
Amisa Hussein, Anastaz Katunzi, Anna Mwaisula, Belina Nyamwihula,
Donisia Minja, Fatuma Maonyo, Happiness Mwaipaja, Latifa Salum, Maimuna
Kaimu, Najiat Idrisa, Neema Kiniga, Rehema Rhamia, Sada Hussein, Shelda
Mafuru, Stumai Athuman, Tatu Salum, Theresa Kashilim na Vumilia Maarifa.
Boniface Wambura Mgoyo
Kaimu Katibu Mkuu
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
Category: tanzania
0 comments