TANZANIA BARA YACHAPWA NA ZAMBIA, YASHIKA NAFASI YA NNE CHALENJI

Unknown | 8:21 AM | 0 comments

 

 

Baadhi ya wachezaji wa Tanzania Bara 'Kilimanjaro Stars'.
Timu ya taifa ya Tanzania Bara 'Kilimanjaro Stars' imeshika nafasi ya nne michuano ya Kombe la Chalenji 2013 iliyofanyika nchini Kenya baada ya kufungwa na timu ya Zambia kwa penalti 6-5. Dakika 90 za mchezo zilimalizika kwa bao 1-1.
Bao la Zambia lilifungwa na Ronald Kampamba katika dakika ya 51 kabla ya Kili Stars kusawazisha kupitia kwa Mbwana Samatta dakika ya 65 kipindi cha pili.
Wachezaji wa Kilimanjaro Stars waliopata penalti ni Mbwana Samatta, Erasto Nyoni, Himid Mao, Amri Kiemba na Ramadhan Singano 'Messi'. Waliokosa ni Haruna Chanongo, Mrisho Ngassa na Kelvin Yondani.
GPL

Share story hii kupitia>>>>>> :
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

Category:

0 comments