STARS YAIVUA UBINGWA UGANDA, YATINGA NUSU FAINALI CHALENJI

Katika mchezo huo uliopigwa katika Uwanja wa Manispaa ya mji wa Mombasa nchini Kenya, Uganda ndio waliokuwa wa kwanza kupata bao la kuongoza likifungwa na Daniel Sserunkuma katika dakika ya 16 akimalizia krosi ya Khamis Kiiza, bao ambalo halikudumu sana kabla ya Mrisho Ngassa kuisawazishia Stars kwa shuti kali 18.
Baada ya bao hilo Stars walikuja juu na kufanikiwa kupata bao la pili likifungwa na Ngassa kwa mpira wa adhabu uliojaa wavuni katika dakika ya 39, matokeo ambayo yalidumu mpaka mwisho wa kipindi hicho cha kwanza.
Kipindi cha pili Stars inayofundishwa na kocha Kim Poulsen, raia wa Denmark, ilipata pigo katikati ya kipindi hicho baada ya kiungo wake Salum Abubakar 'Sure Boy' kutolewa kwa kadi nyekundu baada ya kucheza rafu, ambapo nafasi hiyo iliwapa nguvu Uganda kupata bao la kusawazisha kupitia Martin Mpuga matokeo ambayo yalibaki hivyo mpaka mwisho wa mchezo na kuzipeleka mpaka kwenye matuta.
Katika mikwaju ya penalti Ivo alikuwa shujaa baada ya kucheza penalti mbili za Waganda ya beki Khalis Alucho na ile ya mwisho iliyopigwa na Sserunkuma ambayo ndiyo iliyoivusha stars.
Ifuatayo ni orodha ya waliopiga penalti katika mchezo huo.
Stars Uganda
Erasto Nyoni (kosa) Godfrey Walusimbi (kosa)
Mbwana Samatta (kosa) Emanuel Okwi (pata)
Amri Kiemba (pata) Khalis Alucho (kosa
Athuman Idd (pata) Hamis Kiiza (pata)
Kelvin Yondani (pata) Sserunkuma (kosa)
Habari na Khatimu Naheka / GPL
Category: tanzania
0 comments