CHELSEA YAPIGWA NAYO, LIVERPOOL YAUA 4-1, SYAREZ APIGA MBILI, MAN CITY DROO
BAO
la dakika ya 90 la Oussama Assaidi, limezamisha Chelsea mbele ya Stoke
kwa mabao 3-2 huo ukiwa ushindi wao wa kwanza katika Ligi Kuu ya England
dhidi ya The Blues ndani ya miaka 38.
Winga
huyo wa mkopo kutoka Liverpool, aliingia uwanjani akitokea benchi
zikiwa zimesalia dakika sita na kufunga bao hilo muhimu lililmtoa kichwa
chini kocha Jose Mourinho Uwanja wa Britannia.
Mabao
ya Chelsea yalifungwa na Andre Schurrle dakika za tisa na 53, wakati
mabao mengine ya Stoke yalifungwa Peter Crouch dakika ya 42 na Ireland
dakika ya 50.
Kocha Jose Mourinho akiwa hana raha baada ya kipigo
Wachezaji wa Chelsea wakiwa hawaamini macho yao
Katika
mchezo mwingine wa ligi hiyo, mshambuliaji Luis Suarez ameendelea
kung'ara baada ya kufunga mabao mawili katika ushindi wa 4-1 nyumbani
dhidi ya West Ham.
Suarez
alifunga mabao yake dakika za 81 na 84, wakati mengine yalifungwa na
Demel aliyejifunga dakika ya 42 na Sakho dakika ya 47, huku la kufutia
machozi la wageni likifungwa na Skrtel aliyejifunga pia dakika ya 66.
Nayo
Manchester City imelazimishwa sare ya 1-1 na Southampton ugenini,
Sergio Aguero akitangulia kufunga dakika ya 10 kabla ya Dani Osvaldo
kuwasawazishia wenyeji dakika ya 42.
Mkali kweli: Luis Suarez (wa pili kulia) akipongezwa na wenzake
Suarez akishangilia
Suarez akitafuta mbinu za kumtoka beki wa West Ham
Sergio Aguero akipongezwa na wenzake baada ya kuifungia bao la kuongoza Mancester City
Category: uingereza
0 comments