Mechi ya Kilimanjaro Stars na Harambee Stars yasogezwa mbele.
Mchezo
 wa nusu fainali ya michuano ya GOTV SENIOR CECAFA CHALLENGE CUP 
unaozikutanisha timu mwenyeji The Harambee Stars ambayo ni timu ya taifa
 ya Kenya na Tanzania The Kilimanjaro Stars uliokuwa uchezwe kwenye 
uwanja wa Kenyatta huko Machakos saa 10 jioni kwa muda wa Afrika 
mashariki umesogezwa mbele baada ya mvua kubwa iliyonyesha kwenye uwanja
 huo kufanya mazingira ya mchezo kuendelea kuwa magumu.
Mchezo
 huo umelazimika kuhamishwa toka kwenye uwanja huo wa machakos hadi 
uwanja wa nyayo Nairobi ambapo sasa utapigwa saa 12 jioni .
Nusu fainali nyingine kati ya Zambia na Sudan inatarajia kuanza dakika chache zijazo kwenye uwanja wa Manisapaa huko Mombasa.
Category: tanzania
 



 
 
 
0 comments