HARUNA MOSHI "BOBAN" ATEMWA TENA
Makamu
Mwenyekiti wa Coastal Union Steven Mnguto timu yenye makao yake makuu
pale 96.o Tanga ame-amplify taarifa zinazomhusu mwanasoka Haruna
Moshi’Boban’ kuhusu mkataba wao na Boban.
Coastal
Union wamesema hawatomuongezea mkataba mshambuliaji Haruna Moshi
‘Boban’ kutokana na kuwa na utovu wa nidhamu.Steven Mnguto alisema mpaka
sasa mshambuliaji huyo hajaripoti kambini kuanza mazoezi na wenzake na
hajatoa taarifa yoyote.
Mnguto
ameongeza kwa kusema kuwa kwa tabia aliyoionyesha ni ngumu kumuongeza
mkataba mshambuliaji huyo aliyebakiza miezi sita tu katika mkataba wake
unaomalizika mwishoni mwa msimu huu.Kutokana na kutojiunga na kikosi
hicho mpaka sasa.
Boban atakatwa mshahara wake wa mwezi huu kwa kuwa hajaufanyia kazi
yoyote tokea alipotakiwa kujiunga na wenzake tarehe 1 Desemba mwaka
huu,mbali na Boban adhabu ya namna hiyo pia itamkuta kiungo Jerry Santo
ambaye ni raia wa Kenya kutokana na kutotoa sababu zozote za kuchelewa
kujiunga na wenzake kambini.
‘Ni bora tukapandisha vijana wetu wa U20 kwa kuwa tunajua
watatusaidia na wana nidhamu ya hali ya juu kuliko hawa ambao ni wazoefu
lakini wanatusumbua upande huo’.
‘Hatuwezi kumuongeza mkataba mtu ambaye tunaona kabisa nidhamu yake
haituridhishi kama timu na hajatoa hata taarifa yoyote. Wa nini mtu
kama huyo? Sisi tunaangalia maslahi ya timu ili ifanye vizuri’. .
Kwenye kumbukumbu Boban aliwahi kuondolewa kwenye kikosi cha timu ya
Simba ambacho alikuwa amekitumikia kwa muda mrefu kutokana sababu za
kiutovu wa nidhamu.
Category: tanzania
0 comments