MABOMU YA MACHOZI YARINDIMA TAIFA BAADA YA KAGERA SUGAR KUSAWAZISHA BAO KWENYE MCHEZO DHIDI YA SIMBA

Unknown | 10:23 PM | 0 comments


Hamis Tambwe analiipatia bao la kwanza Simba katika dakika ya 45 kipindi cha kwanza mwishoni baada ya Tambwe kumchambua beki wa Kagera Sugar na kumfunga kipa wa Kagera Sugar
Kipindi cha pili dakika za nyongeza 90+4 Salum Kanoni anaisawazishia bao Kagera sugar na kufanya 1-1 dhidi ya wenyeji Simba kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Kiwango cha wenyeji Simba wakimaliza mtanange wakiwa na 48% na Kagera Sugar wakiwa juu kwa kiwango cha 52%.
Baada ya Kagera Sugar kusawazisha bao hilo kukatokea hali mbaya uwanjani kwa MASHABIKI KUANZA KUNG'OA VITI NDIPO ASKARI WAKALAZIMIKA kutumia mabomu ya machozi kuwatawanya

Polisi wakiwafuata mashabiki wa Simba ambao walikuwa wanang'oa viti

Simba sasa wanafikisha pointi 21 wakiendelea kukaa nyuma ya Azam FC,Mbeya City wenye pointi 23 na Yanga wenye pointi 22 huku Simba akicheza mchezo mmoja zaidi.
Mpaka viti vinavunjwa na mabomu yanaanza kupigwa Simba na Kagera walikuwa wamefungana bao 1-1.
Kagera ambao walikuwa nyuma kwa bao 1-0 lililofungwa na Amisi Tambwe katika kipindi cha kwanza, walipata bao la kusaweazisha kupitia kwa Kanoni kwa njia ya panalti baada ya Joseph Owino kumwangusha Daudi Jumanne katika eneo la hatari.

Share story hii kupitia>>>>>> :
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

Category:

0 comments