Home �
tanzania
� MABINTI WA KIBONGO WAWAFUMUA MSUMBIJI 10-0 TAIFA
Unknown |
9:55 PM |
0
comments
|
Wachezaji wa Tanzania wakishangilia mabao 10-0 |
Na Mahmoud Zubeiry, Dar es SalaamTIMU
ya soka ya taifa ya wanawake kwa vijana chini ya umri wa miaka 20, The
Tanzanites imeifunga Msumbiji mabao 10-0 katika mechi ya kwanza ya
raundi ya Kwanza ya Kombe la Dunia kwa mabinti wa umri huo, Uwanja wa
Taifa, Dar es Salaam jioni ya leo.Katika mchezo huo uliohudhuria na mashabiki wachache mno, hadi mapumziko, tayari Tanzanites walikuwa mbele kwa mabao 5-0.
|
Neema
Paul kushoto akishangilia na Theresa Yona baada ya kuifungia bao la
kwanza Tanzania katika ushindi wa 10-0 jioni hii Uwanja wa Taifa, Dar es
Salaam. |
Bao
la kwanza lilifungwa dakika ya sita na Neema Paul aliyeunganisha pasi
ya Theresa Yona, kutoka wingi ya kushoto, wakati mfungaji bora wa
michuano ya kimataifa ya Airtel Rising Stars iliyofanyika mwaka huu
Nigeria, Shelder Boniface alifunga la pili dakika ya 24 baada ya
kupangua ngome na kumpiga chenga hadi kipa.Deonesia
Daniel akafunga bao la tatu kwa shuti kali la mpira wa adhabu
lililotinga moja kwa moja nyavuni dakika ya 32 na dakika ya 41, Amina
Ali akafunga la nne kwa shuti kali kutoka nje ya eneo la mita 18.
|
Wachezaji wa Tanzania wakishangilia mabao 10-0 |
|
Shelder Boniface akichezewa rafu na beki wa Msumbiji, Esperanca Malaita |
|
Winga wa Tanzania, Theresa Yona akimtoka beki wa Msumbiji, Esperanca Malaita |
|
Theresa amepiga krosi |
|
Shelder Boniface alifunga bao tamu sana, akipiga chenga mabeki watatu na kipa wao |
Shelider Boniface alifunga bao ambalo lingekuwa la tano dakika ya 45, lakini refa Ines Niyonsara wa Burundi akakataa.Kipindi
cha pili The Tanzanites inayofundishwa na Rogasian Kaijage ilirudi na
moto wake na kufanikiwa kupata bao tano, mfungaji Neema Paul
aliyeunganisha krosi ya Theresa Yona.Hatimaye Shelder alifunga bao la sita dakika ya 80 akimalizia mpira uliotemwa na kipa kufuatia shuti la Stumai Abdallah. Dakika ya 82 Tanzania ikapata bao saba kupitia kwa Amina Ali aliyefumua shuti kutoka katikati ya Uwanja.
|
Kiungo wa Tanzania, Amina Ali akipambana na kiungo wa Msumbiji, Deolinda Gove |
|
Theresa Yona alikuwa mwiba mkali leo kwa Msumbiji |
|
Amina Ali akiwaonyesha kazi wachezaji wa Msumbiji |
|
Kikosi cha Msumbiji leo |
|
Kikosi cha Tanzania leo |
|
Mashabiki wakiisapoti timu ya Tanzania leo |
Tanzanites
walipata bao la nane dakika ya 86 kupitia kwa Deonesia Daniel
aliyefunga kwa mkwaju wa penalti, baada ya Shelder Boniface kuangushwa
kwenye eneo la hatari.Dakika
ya 89 Tanzania ilipata bao tisa kupitia kwa Amina Ali tena, ambaye
alikuwa nyota wa mchezo huo. Stumai Abdallah akaifungia Tanzania bao la
10 dakika ya 90.Kikosi
cha Tanzania kilikuwa; Celina Julius, Stumai Abdallah, Maimuna
Said/Amina Hebron dk60, Fatuma Issa, Anastazia Anthony, Deonisia Daniel,
Vumilia Maarifa, Amina Ali, Neema Paul, Shlder Boniface na Theresa
Yona.Msumbiji;
Paulina Jambo/Catarina Francue dk50, Esperanca Malaita/Delice Assane
dk52, Felismisa Moiane, Emma Paulino, Gilda Macamo, Deolinda Gove,
Jessica Zunguene, Cidalia Cuta, Nelia Magate, LonicaTsanwane na Onesema
David.
Share story hii kupitia>>>>>> :
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
Category:
tanzania
0 comments