NIGER MABINGWA TENA AIRTEL RISING STARS
Na Iwedi Ojinmah,
TIMU
ya Niger imefanikiwa kutetea Kombe la vijana chini ya umri wa miaka
Airtel Rising Stars jana baada ya kuifunga Zambia kwa penalti 7-6.
Pamoja na mvua, kulikuwa kuna watu wengi uwanjani na Niger ilipata bao la mapema la kuongoza, lakini Zambia wakawasazisha zikiwa zimesalia dakika saba.
Ikumbukwe Niger iliwatoa wenyeji, Nigeria kwa penalti 8-7 wakati Zambia iliitoa Tanzania kwa mabao 4-3 katika Nusu Fainali juzi.
Category: tanzania
0 comments