Mashindano ya Miss Universe Tanzania 2013 yaanza rasmi kwa warembo kuingia kambini

Baada
ya usaili wa kumtafuta mrembo wa kurithi taji la Miss Universe Tanzania
kumalizika, kambi ya warembo kwa ajili ya kinyang’anyiro cha kumtafuta
mrithi wa taji la Miss Universe Tanzania 2013 imeanza rasmi.
Kambi
hii ambayo imejumuisha warembo 15 kutoka mikoa nane ya Tanzania itakaa
kwa muda wa wiki moja katika hotel ya Urban Rose kabla ya kumpata
mshindi siku ya fainali ambapo itakuwa tarehe 27 mwezi Septemba mwaka
huu katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa.
Ukilinganisha
na miaka mingine mashindano ya mwaka huu yatakuwa tofauti kidogo ambapo
ukiondoa kugombania taji kubwa la Miss Universe Tanzania kulikuwa na
washindi wa pili na watatu. Mwaka huu mshindi mwingine atavikwa moja kwa
moja taji la Miss Earth Tanzania na Mshindi wa tatu bora ndio atakua
runner up.
Warembo
watakaochuana kuwania taji hilo ni kama ifuatavyo na mikoa waliyotoka
kwenye mabano. Aziza Victoria(Dar es Salaam) , Irene Nsiima (Dar es
Salaam), Betty Boniface(Dar es Salaam), Kundi Mlingwa(Dar es Salaam),
Mariam Ngwangwa(Dar es Salaam) , Consolata Mosha( Mwanza), Agnes
Thobias, Dinah David ( mbeya), Upendo Dickson (Dar es Salaam), Naomi
Kisaka(Dar es Salaam), Glady Msemo(Dar es Salaam) , Vestina Mhagama(Dar
es Salaam) , Angela Lutataza(Dar es Salaam) , Clara Noor( Mwanza), Sasha
Lukiko(Dar es Salaam).
Timu
ya Compass Communications ilizunguka takriban Mikoa 8 ya Tanzania
kufanya usahili kwa kila mkoa ili kupata wawakilishi wa mikoani katika
kinyang’anyiro hiki. Mikoa hiyo ni pamoja na Mwanza, Arusha, Mtwara,
Manyara, Mbeya, Dodoma, Kilimanjaro na Dar es Salaam. Jumla ya washiriki
15 wataingia kambini kuchuana kumpata Mwakilishi wa Tanzania katika
fainali za dunia zitakazofanyika nchini Moscow,Urusi.
Mashindano
ya Miss Universe kwa hapa Tanzania yalianza rasmi mwaka 2007 ambapo
Tanzania iliwakilishwa na Flaviana Matata na kufanikiwa kuingia katika
kumi bora na mwaka 2008 yaliwakilishwa na Amanda Ole Sulul, 2009
yaliwakilishwa na Illuminata James ambapo mwaka 2010 mrembo Hellen
Dausen ndiye aliyepokea kijiti, 2011 Nelly Alexandra Kamwelu na
anayekabidhi taji mwaka 2012/2013 ni Winfrida Dominique.
Mashindano
ya Miss Universe yamedhaminiwa na Hifadhi za Taifa (TANAPA), Fastjet,
Mohamed Enterprises (MeTL) na Wadhamini wenza(Parters) ni CocaCola,
Missie Popular Blog, Healthy Beauty Clinic, Beauty Point, Sia Couture,
Seif Kabelele Blog, AZH Photography.com na Adams Digicom
Category: tanzania
0 comments